Select Menu

News

TAMASHA LA MAOMBI

TAMASHA LA MAOMBI

UBUNGE

UBUNGE

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

JIFUNZE KIFARANSA

JIFUNZE KIFARANSA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » 07.12.2016: MCH. KOMBA KUTOKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI AWASHA MOTO USIOZIMIKA KATIKA SHILOH TANZANIA 2016 NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Sanga Rulea 1:11 PM 0


Mch Komba wa kanisa la Mlima wa Moto Dodoma siku ya Jumatano aliweza kutoa ujumbe ambao tunauandaa kwaajili yako. Ujumbe huu uligusa maisha ya watu. Mungu anamtumia mtumishi huyu kwa njia ya tofauti sana. Ni mchungaji ambaye amejishusha kwa kazi ya Bwana na pia kanisa lake limefuata tabia yake. Na hii inatoka na yale mafuta ambayo Mungu ameweka ndani yake.

Mch. Komba na baadhi ya waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Dodoma waliamua kuacha kazi zao zote na kuungana na waumini wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kushiriki baraka za SHILOH. Kumbuka kwa mawaka huu shiloh imebeba ujumbe unaosema, "MOTO USIOZIMIKA", kwahiyo mch. Komba na waumini wake wakaona sio vyema wakakosa kupokea baraka hizi za Shiloh ili watakapoondoka kuelekea Dodoma wakaondoke na na ule Moto Usiozimika ambao utaunguza uchafu na kazi zote za shetani kwa mwaka mzima wa mwaka 2016.

Sio rahisi kabisa kuona mtu anaacha kazi zake na kusafiri safari ya mbali kuja kusikiliza sauti ya Mungu kupitia watumishi wake aliowaweka duniani kwa kazi yake. Kitendo cha hawa waumini kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam kinaonyesha ni jinsi gani walivyo na kiu ya kumjua Mungu na kumtafuta. Wamejinyima na vingi wakaona ngoja wajichange wafike Mlima wa Moto Mikocheni "B" kupokea baraka za Mungu. Bwana hatawapungukia daima.

Sasa na wewe waweza kuungana na hawa ndugu zetu kufika katika nyumba ya Bwana. Uamuzi wako na imani yako vyaweza kuwa mchango mkubwa sana wa kutatua shida yako. Ukiamini na kuchukua maamuzi magumu ya kufika kanisani katika Shiloh hii na kuyashika yale ambayo watumishi wa Mungu wameyaandaa kwaajili yetu basi utaona mkono wa Mungu ukiwa juu yako.

Kupitia SHILO TANZANIA 2016 utaona huruma za Mungu juu yako, utaona upendo wa Mungu juu ya familia yako na kazi yako. Mungu anakwenda kuondoa stress zako, shida zako, magonjwa yako, mapungufu katika uchumi wako na kila kitu kinachokusumbua kinaenda kutoweka kwa jina la Yesu Kristo.

Unatakiwa kujiuliza kwanini wengine wanafanikiwa na wewe hufanikiwi wakati wote mlizaliwa mkiwa hamna kitu, mkitegemea misaada kutoka kwa wazazi wenu, lakini leo wewe uko chini kiuchumi na mwingine yuko juu. Ukiona hivyo ujue kuna udhaifu sehemu fulani katika fikra zako. Njoo Shiloh sasa ufunguliwe fikra zako na nafsi yako iliyotekwa na shetani. Mungu akubariki sana.

Ratiba ya Shiloh ni kama ifuatavyo. Kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana ni maombezi na saa 9 mchana hadi 12 jioni na ibada kuu ya Shiloh. Wahubiri ni wengi sana kwani kuna Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Bishop Dustani Maboya, Mch. Komba, Mch. Simtomvu, Mch. Wambura, Mch. madoshi, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Noahl Lukumay, Mch Karisto Kyando, Mch. Dickson, Mch. Francis Machichi na wengine wengi. Mungu awabariki sana.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


kulinia ni Mch. Prisca wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"Kutoka kulia ni Mch. Francis Machichi, Mch. Noah Lukumay na Bishopd Dunstan Maboya

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS