MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.12.2016: BISHOP DUNSTAN MABOYA AKIHUBIRI SIKU YA ALHAMISHI YA SHILOH TANZANIA NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mungu anazidi kufanya mambo ambayo yanamchanganya shetani kupitia mtumishi wake Bishop Dunstan Maboya kutoka Arusha ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Yaani tunatamani sana kukupa kile alichokihubiri siku hii ya Alhamis 08.12.2016, lakini tunakuahidi kuwa tutakuletea mahubiri yake kupitia akaunti yetu hii. Kipindi hiki cha SHILOH TANZANIA 2016 ndani ya siku 8 hizi za Moto usiozimika, Mungu anazidi kumwachia upako Bishop Dunstan Maboya na yeye amekuwa mwaminifu kwani amekuwa akiachilia upako kwetu tuliyebahatika kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kushiriki SHILOH ambayo itahitimishwa siku ya Jumapili 11.12.2016.


Neno langu kwako ni kukuomba ufike katika ibada ya Shiloh inayoendelea katika kanisa hili, maana leo hii kuna Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini ambaye Mungu amemubariki kiuchumi nchini Afrika Kusini na leo atafundisha jinsi ya kujikwamua katika umaskini na kuachia ule upako alionao juu ya masuala ya kiuchumi. Pia amesema Neno la Mungu litakuwa ndio msingi wa yote kwani utajifunza mengi kuhusu Mungu na utatoka ukiwa tofauti sana. Ibada itaanza saa 9 mchana hadi 12 jioni na kipindi cha maombezi ni saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana..Usikose