TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.12.2016: REV. ELIAS NDEDA KUTOKA AFRIKA KUSINI AFUNDISHA JINSI YA KUTOKA KATIKA UMASKINI NDANI YA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hatimaye Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini siku ya alhamis 08.12.2016 aliweza kuhubiri kwa mara ya kwanza tangia SHILOH ianze ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Rev. Ndeda alisema kwa siku hizi tatu atakazohubiri atahakikisha Mungu anafanya jambo juu ya uchumi wako, alisema yeye Mungu amembariki sana tena kiuchuni nchini Afrika Kusini na amekuwa na maisha ambayo yanastahili mtu aliyeokoka kuyaishi. Kwahiyo kwa siku hizi tatu atafundisha kujikwamua kiuchumi na baadae ataachilia upako wa mafanikio ambao utaenda nao kwa mwaka mzima wa 2017. Alisema, Mungu anapenda kuona mtu aliyeokoka kuishi maisha ya furaha na ndio maana katika Biblia yake takatifu amesema, tutamiliki kila kitu chini ya dunia hii.

Usikose ibada ya leo itakkayoanza saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana ambapo watu watafanyiwa maombezi na saa 9 mchana hadi 12 kutakuwa na ibada Kuu ya Shiloh Tanzania ambapo Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Bishop Dunstan Maboya, Mch. Noah Lukumay, Mch. Francis Machichi, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Komba, Mch. wambura, Mch. Simtomvu, Mch. Mapunda, Mch. karisto Kyando, Mch. Sebastian na wachungaji mbalimbali kutoka katika mikoa 24 ya Tanzania watafundishi Neno la Mungu na kukuombea. USIKOSE BARAKA HIZI, NJOO NA MWENZAKO.