RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.12.2016: REV. ELIAS NDEDA KATIKA SHILOH TANZANIA 2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" ACHUKIZWA NA UMASIKINI KWA WATU WALIOKOKA

Rev. Elias Ndeda kutoka Afrika Kusini siku ya Ijumaa ya SHILOH Tanzania 09.12.2016 aliweza kufundisha na kuhubiri juu ya watu kuondokana na umaskini. Alisema anakerwa sana anapoona watu waliokoka wanakuwa na maisha magumu wakati wao ndio walitakiwa kutawala kila kitu hapa duniani. Kingine alichowasisitiza watu ni kufanya kazi kwa bidii na kuachana na uvivu kwani uvivu ni chanzo cha umaskini. Rev. Ndeda alisistiza watu kumtumikia Mungu kwa Roho ya kweli na sio nusu nusu kwani kwa kufanya hivyo Mungu ataachilia mafanikio katika maisha yao.

Siku ya Jumapili 11.12.2016 ambayo ni siku ya hitimisho la SHILOH Tanzania atakuwepo Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwahiyo usikose baraka za Mungu kupitia mtumishi wake kutoka Afrika kusini. Nasi tupo katika maandalizi ya kukuletea somo alilofundisha siku ya Ijumaa. Endelea kufuatilia post zetu. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu akubariki sana...