RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.12.2016: MIOYO YA WATU YAPONYWA KUPITIA UIMBAJI SIKU YA JUMAPILI YA KRIMASI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hakika Mungu anazidi kulikumbuka kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Upendo wake unashangaza walio wengi, Mungu wetu anahuruma jamani. Mwokozi wetu anajua yaliosirini mwa mtu kwani kupitia uimbaji tunaona akifanya makuu kwa watu wake katika kanisa la Mlima wa Mungu..

Martha Komanya

 Inakupasa sasa kumuachia Mungu aongoze maisha yako kwani yeye ni rafiki wetu wa kweli. Dhamani ya wokovu na gharama ya maisha yetu anayejua ni mwokozi jamani. Tumemuona Mungu akifanya makubwa kupitia uimbaji siku ya Jumapili ya Krismasi 25.12.2016 wakati Praise and Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" ikiongozwa na Martha Komanya. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakare

Nyimbo zao ziligusa nafsi za watu na kujikuta watu wakisimama kwenye viti vyao na kuanza kumchezea Mungu huku wakirukaruka kwa furaha kuashilia jinsi gani Mungu alivyokuwa akiwashughulikia kuponya mioyo yao iliyogua kwa muda mrefu na magonjwa kutoka kwa shetani.
Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"

Inakupasa sasa kumuomba Mungu sana afanye ibada ndani yako ili uweze kumsifu na kumwabudu kwani yeye ndiye anayekupa mamlaka na nguvu ya kumtumikia kama utamruhusu kuwa ndani yako. Muombe Mungu utumike chini ya pendo lake. Mungu ameshakupa nguvu ila ni wewe kuchukua uamuzi wa kumtumikia. 



Tunawashukuru waimbaji hawa kwani wao walipoona wana nguvu na mamlaka wakaamua kumsifu Mungu siku ya Krismasi na kupitia sifa zao watu waliweza kuambukizwa upako walikokuwa nao ambao ulishababisha maisha ya wengine kubadilika na kuongeza ila hali ya kuwa na hofu ya Mungu.

Hakika nyimbo zenye upako zimekuwa zikigusa maisha ya watu kupitia waimbaji hawa. Tuna kila sababu ya kuwaombea ili wazidi kufanya kazi ya Bwana bila kuchoka wala kukatishwa tamaa. Pia tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" na siku za katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 12 au 1 jioni. Mungu akubariki sana














 Mch. Stanley Nnko