MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

25.12.2016: MIRIAM JACKSON AACHA ALAMA YA KUKUMBUKWA KATIKA IBADA YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI YA KRISMASI

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Tanzania Miriam Jackson ambaye amekuwa balozi katika kumzungumzia Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anapokuwa katika huduma zake nje ya Tanzania,  siku ya Jumapili ya Krismasi 25.12.2016 aliweza kufika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwaajili ya kumtukuza Yehova kwa njia ya uimbaji. Miriam Jackson alisema, mara nyingi huwa anajivunia sana anapokuwa nje ya Tanzania akifanya huduma yake kwa kuwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Sasa ngoja nikupe baadhi ya maneno yaliyomo katika wimbo wake wa  “NI BWANA” ambao amemshirikisha Goodluck Gozbert ambao aliuimba siku ya Jumapili, maneno hayo ni haya hapa ,“Nimemuona Bwana maisha mwangu, nimemuona Bwana anayeweza, yaliyoshindiaka leo nayaweza maana ninaye Bwana Mungu anayeweza. Walioitwa tasa majina yao leo yamebadilika  wanaitwa mama kwasababu wamemuona Bwana, walioshindwa leo wanaweza kwani yeye ndiye MUNGU na sasa wanaweza. Mungu anaweza kufanya hata kwako unachotakiwa kufanya ni kumuita Yeye . Mungu aliyefanya kwao na kwako anaweza kwani yeye ni Yehova, ni Mungu anayeweza.

Mh..kichwa changu na mawazo yangu, mimi ninakushukuru Mungu, kwani moyo wangu unabubujika, upendo wako Mungu unanifunika bure kabisa. Kwa hadhi yangu, maneno yako, upendo wako havilingani, umenipendelea Yahweh . Ooh baba asante kwa jana, asante kwa leo, asante kwa kesho ewe Mungu wangu."

 Miriam Jackson