RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

04.12.2016: BAADHI YA WATU WAKIINGIA KATIKA KUSANYIKO LA WATOTO WA MUNGU SHILOH TANZANIA 2016 KATIKA KANISA LA MLIMA W MOTO MIKOCHENI "B"


Siku ya Jumapili 04.12. 2016 baadhi ya watu waliweza kujitokeza kushiriki kongamano Shiloh Tanzania 2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gerturde Rwakatare. Hizi ni baadhi ya picha za watu wakiingia kanisani. Shiloh hii imezinduliwa rasmi na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wakishirikiana na Bishop Damsatn Maboya siku ya Jumapili.

Kusanyiko hili la SHILOH litafanyika kwa muda wa siku 8 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana kutakuwa na maombezi na baada ya hapo kutakuwa na Ibada ya Shiloh kuanzia saa 9 mchana hadi saa 12 jioni.

Usikose siku hizi 8 za Moto Usiozimika, kwani ni siku ambazo Mungu ataongea na wewe kupitia watumishi wake akiwemo Rev. Ndeda kutoka Afrika kusini, Bishop Dansatn Maboya kutoka Arusha, Bishop Dr. Getrude Rwakatare mwenyeji (Dar), Mchunganji Kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" Noah Lukumay na wengine wengi kutoka mikoani. Waimbaji ni Masanja, Christina Shusho, Bahati Bukuku. Usikose


 







Mafuta ya upako maji ya upako, bannners, maji ya upako yametengenezwa na Rumafrica