MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE NA MCH. NOAH LUKUMAY KUANGUSHA NGOME ZA YERIKO ZILIZOFUNGA MAFANIKIO YAKO YA KIMWILI NA KIROHO JUMATANO HII 21.12.2016

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wanakualika sana katika ibada ya Jumatano 21.12.2016, ambayo ni ibada ya tofauti sana ya KUANGUSHA MGOME ZA YERIKO. Ukipata muda soma Joshua 6:1. Yawezekana ukuta wako katika maisha yako ni roho ya madeni, umaskini, misiba, magonjwa, uzinzi, kukosa pesa, kukosa kazi, kukosa promosheni, kutosoma Nenola Mungu, kibuli, kukata tamaa, ndoa kukosa amani, umalaya, uongo, mikosi, ajali, kutekwa nafsi, majini, mapepo, kulogwa, kukosa mume/mke, kukataliwa, umasiki  na mengine mengi kama hayo. Jumatano hii watumishi wa Mungu wameomba juu yako kuhakikisha roho za kukurudisha nyuma na kukukosesha raha zinakwenda kuangamia kwa damu ya Yesu Kristo.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mungu anaweza kufanya njia pasipo na njia kama ukiamini na kutii sauti ya Mungu. Kupitia ibada hii unaombwa sana kushika sana na kuheshimu sauti ya watumishi wa Mungu na kitendo hicho kitafanya kukuondoa katika tope la majaribu yako. Mungu ameweka kitu ndani ya watumishi hawa ili tuweze kupona na kukombolewa.

Sasa Jumatano hii Bwana anakwenda kukushughulikia na kukuweka huru katika dimbwi la maji ulilozama na huna msaada. Umehangaika sana bila kupata majibu, umeombewa sana lakini hakuna lolote, sasa amini leo Bwana anakwenda kukusaidia na kukuokoa kwasababu anakupenda. Jitahidi sana kuchukua maamuzi magumu ya kuacha kazi zako na kukimbilia nyumbani mwa Bwana. Mungu akusaidie sana tukutane Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 mchana hadi saa 12 jioni. Ubarikiwe.