MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AKIWAKISLISHWA NA MGENI RASMI DAVID ROBERT MWAMSOJO WALIVYOWEZA KULA KEKI NA WATOTO KATIKA KUKARIBISHA KRISMASI SIKU YA 22.12.2016Siku ya Alhamisi 22.12.2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lililopo jijini Dar es Salaam akishirikiana na walimu wa shule ya watoto waliweza kuandaa siku maalum ya watoto kutoka sehemu mbalimbali kuja kusherekea siku ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo (Krismasi). Bishop Dr. Gertrude Rwakatare (Superwoman) amekuwa akifanya hivyo kila mwaka kwa watoto kusherekea siku ya kuzaliwa Kristo kabla ya Krismasi kufikia ili watoto waweke uzito umuhimu wa Krismasi pale inapofikia tarehe 25.12. ya mwaka. Na hii inasabaisha watoto kuwa na ile hali kuwa katika uwepo wa siku ya kuzaliwa Yesu Kristo,

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuandaa chakula, vinywaji na pia kulikuwa na zawadi mbalimbali kama vile daftari, kalamu na zawadi nyingi ambazo zilitolewa kwa watoto na FATHER KRISMASI

Katika sherehe hii kulikuwa na mgeni rasmi Bwana David Robert Mwamsojo akiwa ameongozana na mke wake Neema David. Mgeni rasmi aliweza kusikiliza risala ya watoto na baadae aliweza kutoa hotuba yake ambayo iligusa sana watoto na wazazi waliohudhuria sherehe hiyo. Kuna vitu vingi sana mgeni rasmi aliweza kuahidi ikiwa ni pamoja na watoto kupata muda wa kushiriki Ibada Kuu ya Malima wa Moto Mikocheni "B", kuwa na michezo mbalimbali siku za wikendi kama Jumamosi kila baada ya mwezi itakayowasaidia watoto hawa kufahamiana na kusababisha kupenda kwenda kanisani, kufanya mazoezi mbalimbali kwaajili ya afya na sio kutumia muda mwingi sana kukaa chini wakicheza game. Pia aliwashauri kama watacheza game basi wapende kucheza games kwa muda mchache sana na sio kukaa muda mrefu kucheza game, Aliwaomba wanapotaka kucheza game waombe kibali kutoka kwa wazazi wao ili wawaonyeshe games ambazo zinaendana na uwezo wao na sio kila game ni ya kucheza kwa wato. Alisisitiza sana watoto kupenda kusooma vitabu mbalimbali ili kupanua uwezo wa kufikiri na kujua mengi, wapende sana elimu na bila kusahau kusoma Neno la Mungu. Aliwaomba watoto kuwa na upendo, wapendane wao kwa wao na kuwapenda wazazi wao, kwasababu Yesu Kristo alikuwa n mtu wa upendo alipenda kila mtu na ndio maana mpaka leo tunamkumbuka.

Mgeni rasmi aliwapongeza wazazi kwa kuwalea watoto, aliwashukuru sana walimu ambao wamejitoa kuwafundisha hawa watoto na sasa wamekuwa na ujasiri wa kujua Neno la Mungu na kuwa na ile hofu ya Mungu. Aliwaomba wazidi kuwafundisha na kuwalea hawa watoto ili hata wakiwa watu wazima waweze kuwa watu bora katika jamii.

Mgeni rasmi aliweza kuwalisha keki baadhi ya wazazi na walimu waliofika katika sikukuu hiyi ya kumbukumbu ya kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Watoto waliweza kupata muda wa kuonyesha vipaji vyao kama vile kushika mistari ya Biblia, kutaja vitabu vyote vilivyomo katika Biblia, kuimba, kuigiza, kucheza, mashairi, vitendawili, ngonjera na michezo mbalimbali.

Walimu waliweza kuwashukuru wazazi wa watoto kwa kuwaruhusu kujifunza Neno la Mungu, walimshukuru Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa moyo wake wa upendo wa kutenga muda kwaajili ya watoto kujifunza Neno la Mungu pamoja na kuandaa siku maalum kila mwaka kwaajili ya watoto kusherekea siku ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Hakika ilikuwa siku ya baraka sana. Mungu azidi kuwatunza na kuwalinda walimu wa shule ya watoto na kumbariki mbeba maono Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kuweza kuona umuhimu wa watoto katika kanisa.