RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAMBO YANAYO SAIDIA LUGHA KUKUA



Kuna mambo mbalimbali anayosaidia lugha yetu kukua.

Kutumika katika elimu, Suala hili la elim husaidia lugha yetu kukua na kuendelea kutumika bila kufa. Kupitia utoaji wa elim mbalimbali kwa lugha hii ya Kiswahili ndio sababu ya kukua kwakekwani elim hiyo huanzia shule za msingi ikiwa ndio lugha ambayo hutumika kutolea elim, sekondari huwa ni somo ambalo hufundishwa na vyuo huwa kozi ambayo mtu husomea kwa miaka mitatu.


Uundaji wa vyombo mbalimbali ambavyo husaidia katika ukuaji wa lugha yetu, Kuna BAKITA(Balaza la Kiswahili Tanzania) TUKI(Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili) BAMITA(Balaza la Mitiani la Taifa). Hivi ni baadhi ya vyombo ambavyo husaidia katika suala zima la ukuzaji wa lugha yetu ya Kiswahili.

Uwepo wa vyombo vya habari, Vyombo hivi vya habari husaidia sana katika suala zima la ukuzji wa lugha yetu kwasababu lugha ambayohutolewa huwa ni ya kiswahili hivyo kufanya watu wengi kuelewa ujumbe ambao unatolewa. Mfano kuna redio, televisheni na magazeti. Hivi ni baadhi ya vyombo ambavyo husaidia katika ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya kiswahili.

Suala la Dini, Pia dini inaidia katika uenezaji wa lugha ya kiswahili kwani mahubili hutolewa kwa lugha hii ya kiswahili ambayo hufanya watu kuelewa ujumbe ambao unatolewa. Wakati wa ukoloni pia dini ilisaidia kukuza ligha na kufanya iendelee hadi leo.

Suala la biashara, Pia biashara nayo imesaidia sana katika ukuzaji wa lugha hii ya kiswahili. Biashara ambazo zinafanyika huendeshwa kwa lugha ya kiswahili hivyo hupelekea lugha kukua zaidi. Hata katika kipindi cha wakoloni biashara ilisaidia kukuza lugha ni kwasababu ya luhga iliyokuwa inatumika ni ya kiswahili.