Select Menu

News

UBUNGE

UBUNGE

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

JIFUNZE KIFARANSA

JIFUNZE KIFARANSA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » MAREKANI: WAJUMBE WAIDHINISHA USHINDI WA DONALD TRUMP


Sanga Rulea 1:48 AM 0Wajumbe wa Jopo la Kuamua Mshindi wa Urais nchini Marekani wamemuidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba.

Hii ni licha ya juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia kuingia ikulu ya White House mwezi Januari.

Wiki sita baada ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 8 Novemba, mwanachama huyo wa Republican amepata zaidi ya kura 270 za wajumbe ambazo alikuwa anahitaji kufanya rasmi ushindi wake.
Familia ya Donald Trump: Wake na watoto

Baada ya ushindi huo, Bw Trump ameahidi "kufanya kazi kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote".

Wajumbe walikuwa wametumia ujumbe mwingi kupitia barua pepe na pia kupigiwa simu wakihimizwa kutomuunga mkono bilionea huyo kabla yao kukutana kupiga kura.

Shughuli yao ya kupiga kura kwa kawaida huwa kama shughuli ya kutimiza wajibu tu, ambapo huwa wanamuidhinisha mshindi, lakini mwaka huu uchaguzi umegubikwa na tuhuma za kuingiliwa na wadukuzi kutoka Urusi.
Je wajumbe wanaweza kumpokonya Trump ushindi?
Paul Ryan arejea kwa kishindo

Jimbo la Texas hatimaye lilimuwezesha kufikisha idadi ya kura 270 za wajumbe alizohitaji,, licha ya wajumbe wawili wake kugeuka na kupiga kura kumpinga.

Gazeti la New York Times pia linaripoti kwamba kuna wajumbe wanne wa chama cha Democratic, chake Hillary Clinton, ambao walimpigia kura mgombea mwingine lakini Bi Clinton.

Matokeo ya kura hiyo yatatangazwa rasmi tarehe 6 Januari kwneye kikao maalum cha pamoja cha bunge la Congress.

"Nawashukuru Wamarekani kwa kunipigia kura kwa wingi kuwa rais wa Marekani," Bw Trump alisema kupitia taarifa baada ya matokeo kutangazwa.

"Kwa hatua hii ya kihistoria, tunaweza sasa kutazama mbele na kutarajia maisha ya kufana siku za usoni. Nitafanya kazi kwa bidii kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote," alisema.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS