TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTOTO WA RAIS AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


MSUMBIJI: Mtoto wa Rais wa zamani wa Msumbiji Armando Emílio Guebuza, Valentina Guebuza ameuawa kwa kupigwa risasi leo asubuhi na anayesadikiwa kuwa ni mumewe mjini Maputo nchini humo.

Taarifa za awali zinasema polisi wanamshikilia mume wa marehemu Zofimo Muiuane kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo huku ikielezwa kuwa wawili hao walikuwa wamefarakana tangu wiki iliyopita.


Ms Guebuza mwenye umri wa miaka 36, ameripotiwa kupigwa risasi nyingi sehemu mbali mbali za mwili wake, kabla ya kukimbizwa hospitali ambapo mauti yalimkuta akiwa njiani kutokana na maumivu makubwa, majeraha na vidonda alivyopata kutokana na tukio hilo.

Mnamo mwaka 2013, mwanamama huyo aliwahi kutajwa na Jarida maarufu duniani la Forbes kuwa ni miongoni mwa Wanawake Saba Wachapakazi Barani Afrika akiwekwa kwenye kipengele cha Sekta za Mawasiliano na Benki, pia alikuwa akimiliki makampuni na familia yake yaitwayo Focus 21, Gestão e Desenvolvimento, Lda.

Wanandoa hao walioana mwaka 2014 ambapo sherehe ya harusi yao ilihudhuriwa na wageni zaidi ya 1,700 akiwemo aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, Mfalme wa Swaziland, Mswati wa III na Isabel dos Santos, ambaye ni mtoto wa Rais wa Angolan president. Mwaka jana walibahatika kupata mtoto wa kike.