Select Menu

News

MTUME DR. PETER NYAGA

MTUME DR. PETER NYAGA

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

» » MVUA YAHARIBU MAKAZI YA KAYA ZAIDI YA 100, BUTIAMA


Sanga Rulea 11:30 PM 0


BUTIAMA: Mvua kubwa ambayo imeambatana na upepo mkali, imesababisha maafa makubwa katika vijiji vitatu vya wilaya ya Butiama mkoani Mara na kusababisha nyumba za kaya zaidi ya mia moja zikiwemo nyumba za ibada kubomolewa vibaya na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali, huku idadi kubwa ya ekari za mashamba yenye mazao mbalimbali pia yakiathiriwa na mawe yaliambatana na mvua hiyo.

Akizungumza baada ya kukagua athari ambayo imesababishwa na mvua hiyo, mwenyekiti wa kamati ya maafa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Bi Annarose Nyamubi, akiwa ameambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya Butiama Bw Magina Magesa, wamesema mvua hiyo imesababisha madhara makubwa na kwamba watendaji wa serikali wameanza kufanya tathimini ya kina ili kujua ukubwa wa maafa hayo

Naye diwani wa kata ya Butuguri Bw. Paul Warati, akizungumzia maafa hayo, amesema tathimini ya awali inaonyesha kuwa zaidi ya kaya mia moja,majengo ya taasisi, chakula na mazao mashambani zimeathirika na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali.

Chanzo: ITV

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS