RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI MASHUHURI WA MUZIKI WA INJILI AFRIKA KUSINI AFARIKI DUNIA.


Mwimbaji mashuhuri wa muziki wa Injili Afrika Kusini S’fiso Ncwane amefariki dunia hapo jana baada ya figo zake kushindwa kufanya kazi.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinasema kuwa nguli huyo wa muziki alikuwa akilalamika juu ya ugonjwa wake huo siku chache zilizopita jambo lililopelekea hata yeye kutokufanya vizuri kwenye onyesho lake alilolifanya juma lililopita huko Limpopo.

Ncwane alifariki hapo Desemba 5 muda mfupi baada ya kukimbizwa katika hospitali ya Life Fourways baada ya kulalamika sana juu ya kuumwa.S’fiso Ncwane ambaye amezaliwa mwaka 1979 atakumbukwa zaidi kwa kibao chake Kulingile baba alichokitoa mwaka 2011 na kupata umaarufu mkubwa nchini humo na kumpatia tuzo kadhaa.

Marehemu S’fiso Ncwane ameacha mke mmoja ,watoto wawili pamoja na mama yake mzazi.Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.