TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

PICHA 10: BALOZI WA URUSI NCHINI UTURUKI ALIVYOUAWA NA ASKARI AMBAYE HAKUWA ZAMU

Balozi wa taifa la Urusi nchini Uturuki Andrey Karlov, ameuawa December 19 2016 kwa kupigwa risasi na mtu ambaye alikuwa nyuma yake. Imeelezwa kuwa aliyemshambulia ni afisa wa polisi ambaye hakuwa kwenye zamu wakati balozi huyo alipokuwa anatoa hotuba kwenye maonesho ya picha katika mji mkuu Ankara.
Balozi wa Urusi nchini Uturuki Andrey Karlov,

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuuawa kwa balozi wa taifa lake nchini Uturukini uchokozi ambao lengo lake ni kuvuruga juhudi za kutafuta amani Syria. Kwa upande wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, amesema kuuawa kwa balozi huyo ni shambulio dhidi ya taifa la uturuki.

Picha za video zilimuonesha mshambuliaji, akiwa amevalia suti na tai, akimfyatulia risasi balozi huyo kutoka nyuma, akisema kwa sauti ujumbe kuhusu mji wa Aleppo, Syria,mshambuliaji huyo aliuawa kwa kupigwa risais na polisi.

Taarifa zinasema muuaji ni Mevlut Mert Aydintas ’22’, ambaye alikuwa anahudumu katika kikosi cha polisi cha kupambana na fujo mjini Ankara lakini haijabainika iwapo ana uhusiano wowote na kundi lolote.
Kisa hicho kilitokea siku moja baada ya maandamano kufanyika Uturuki kupinga hatua ya Urusi kumuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad. Recep Tayyip Erdoganalizungumza na Rais Putin kwa njia ya simu, na kwenye ujumbe wa video, alisema wote wawili walikubaliana kisa hicho kilikuwa “uchokozi”.
Nje ya jengo ambalo kumetokea tukio

Mevlut Mert Aydintas aliyemshambulia kwa risasi balozi wa Urusi nchini Uturuki