MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SABABU MANONGA CLASSIC KUTOKWA NA MACHOZI KILA ANAPOUTUMBUIZA WIMBO WAKE WA SINA HOFUHii ni nyingine kali kutoka kwa mwimbaji mashuhuri kutoka jijini Mwanza nchini Tanzania anayeitwa Manonga Classic ambaye hivi karibuni ameachia wimbo uitwao Acha Nikuimbie,taarifa nzuri ikufikie kwamba Manonga kaambatanisha wimbo huu mwingine katika kuufunga mwaka unaoitwa 'SINA HOFU'

Huu ni moja kati ya nyimbo ambazo Manonga ameimba kwa hisia kali na kwa imani kubwa,wimbo unaelezea kuhusu mtu ambaye hana hofu pamoja na kwamba anapita katika mapito makubwa na magumu maishani.

Mara kadhaa Manonga amekuwa akitokwa machozi anapokuwa jukwaani akitumbuiza wimbo huu hari ambayo imekuwa ikiwashangaza wengi,je! ninikinamsababisha kutoa chozi?Promover.com imempata kujibu swali hilo.

Akizungumza na Promover.com Manonga anasema wimbo huo unafanyika sana baraka kila anapouskia na kwa mara kadhaa amejikuta akitokwa machozi kutokana na historia ya wimbo huo.

Anasema aliandika wimbo huo akiwa anapita katika changamoto na misukosuko mikubwa maishani lakini kamwe hakuacha kumtegemea Mungu wa mbinguni

"Wakati naandika wimbo huu nilikuwa na mgonjwa hospitali mtu wa muhimu sana maishani kwangu,wakati nahangaika kumhudumia na kumfariji hospitali kwa wakati huo huo nilitakiwa niingie mtaani kwaajili ya kufanya huduma,kutafta pesa,na mengine mengi, nilipokuwa nikiulizwa nawezaje kufanya yote hayo kwa wakati mmoja wengi niliwajibu Sina hofu naye atanilinda tu,Hakika ni wimbo unaoniteka hisia kila nikiusikia".Anasema Manonga.

Wimbo huu unapatikana kwenye album mpya yake Manonga Classic inayoitwa RUDI ambapo manonga anasema yuko tayari kuutumbuiza wimbo huo na nyingine nyingi zake kali iwapo ataalikwa.Kama unamuhitaji Manonga unaweza kumpata kwa simu namba:0752 690 120