SERIKALI YAFUTA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WALEMAVU

DODOMA: Serikali imebatilisha uamuzi wake wa kufanya maadhimisho ya Siku ya Walemavu Kitaifa Jijini Dar es Salaam na kutoa agizo kwa wakuu wa mikoa yote nchini kufanya maadhimisho hayo katika mikoa yao.

Tamko hilo la serikali limetolewa Mjini DODOMA na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI George Simbachawene na kusisitiza kuwa viongozi wa mikoa na wilaya kusaidia viongozi wa vyama vya walemavu kufanikisha maadhimisho hayo.