TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

SHILOH TANZANIA YAZINDULIWA KWA KISHINDO SIKU YA JUMAPILI 04.12.2016 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Mungu anazidi kufanya mambo makubwa katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni. Tumemuona Mungu akishughurika na Roho za watu kupitia SHILOH iliyozinduliwa siku ya Jumapili katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akishirikiana na Bishop Danstan Maboya. Watu wengi walifunguliwa katika nafsi zao zilizotekwa na adui shetani kupitia maombi ya moto usiozimika yaliyokuwa yakifanyika katika nyumba ya Bwana na watumishi wa Mungu mbalimbali ambao hakika Mungu anawatumia kwa njia ya tofauti sana.

Ibada hii ilihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka pande zote za Tanzania kwa lengo la kuja kumtukusa Mungu katika kusanyiko la watoto wa Mungu la SHILOH.

Kusanyiko hili la SHiloh hufanyika mara moja tu kwa mwaka na mwaka huu limeanza siku ya Jumapili 04.12.2016 na litahitimishwa 11.12.2016 ambapo watu watapokea baraka za Mungu, watafunguliwa katika vifungo vyao, watapokea miujiza yao, wataombewa, wataponywa, wataheshimika, watapata vibali, watainuliwa, watakaa na wakuu, wataongezwa mishahara, watatamani kusoma neno la Mungu, watasamehewa dhambi zao, wataona wepesi wa maisha yao na mambo mengi mema kutoka kwa Bwana.

Watumishi wa Mungu mbalimbali kama Bishop Danstan Maboya, Rev. Ndeda kutoka Afrika Kusini, Mch. Noah Lukumay, Mch. Madoshi, Mch. Kimba kutoka Dodoma, Mch. Sebastian, Mch. Stanley Nnko, Mch. Prisca, Mch. Elizabeth Lucas, Mch. Simtovu na wengine wengi watakuombea katika kongamano hili la kimataifa, utaondoka na kicheko cha kumaliza mwaka kwa Jina la Yesu Kristo. Leo ibada inaendelea saa 9 mchana hadi 12 jioni na pia kuna ibada ya maombezi kila siku saa 4 asubuhi hadi 8 mchana. Mungu akubariki sana.