MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

TWAWEZA: ASILIMIA 88 YA WANANCHI WATAKA BUNGE LIRUSHWE LIVE

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).


DAR ES SALAAM: UTAFITI wa taasisi ya Twaweza umeonyesha kuwa asilimia 88 ya wananchi nchini wanataka majadiliano ya vikao vya Bunge yarushwe moja kwa moja bila kujali gharama yoyote, wakati asilimia 12 tu wakisema wanadhani suala la kubana matumizi ni sababu ya kutorusha vipindi vya bunge moja kwa moja.

Aidha, utafiti huohuo umeonyesha kwamba asilimia 95 ya wananchi wanaunga mkono uhuru wa maoni na kupata taarifa kwani wanasema ni haki yao kuikosoa serikali pale ambapo wanaona imekosea.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam aliposema utafiti huo ni takwimu za sauti za wananchi zinazoonyesha kuunga mkono wajibu wa vyombo vya habari katika kuiwajibisha serikali.

Amesema wananchi pia wanaunga mkono demokrasia kwani takwimu za hivi karibuni zinaonyesha asilimia 69 ya walichagua demokrasia kuliko aina nyingine ya serikali kwa takwimu za mwaka 2014.

Aidha takwimu zinaonyesha asilimia 77 ya wananchi wa kawaida wanatakiwa wawe na uwezo wa kupata taarifa zinazoshikiliwa na mamlaka za umma huku asilimia 23 wakisema ni wale tu wanaofanya kazi kwenye mamlaka za umma ndiyo waruhusiwe kupata taarifa hizo.

Na kwa upande wa asilimia 80 wanasema upatikanaji wa taarifa hizo kwa wananchi utasaidia kupunguza vitendo vya rushwa huku asilimia 20 wakisema watumishi wa umma watatafuta njia nyingine za kuficha maovu yao.

Alifafanua kuwa takwimu hizo ni za hivi karibuni za utafiti zilizokusanywa na Twaweza baada ya kutiwa saini kwa sheria mpya ya huduma za vyombo vya habari.

Na Denis Mtima/GPL