RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: ALICHOKISEMA MMILIKI WA JAMII FORUMS BAADA YA KUPATA DHAMANA LEO

Leo December 19, 2016 kutoka Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es salaam, mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa JAMII FORUMS Maxence Melo ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 5 ambapo baada ya kupata dhamana hiyo Max ameyaongea yafuatayo.

“Nawashukuru mawakili wangu najua wamekuja kwasababu ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari, jukumu hili sio la Max peke yake ni jukumu la wote, Max amekuwa mfano tu wakati mwingine atakuwa mtanzania yeyote anayetaka kutetea uhuru wake, mimi sina shida na vyombo vya dola vinafanya kazi yake” – Maxence Melo