MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

01.01.2016: MCH. PRISCA ASABABISHA WATU KUTOKWA NA MACHOZI KATIKA MKESHA WA KUKARIBISHA MWAKA 2017 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Mch. Prisca wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili ya kwanza ya mwaka 2017 ya tarehe 01.01.2017 katika mkesha wa kukaribisha mwaka 2017 yaani Crossover, aliweza kupata kibali cha kuongoza kipindi cha kusifu na kuabudu akiwa na Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Kupitia sauti ya Mch. Prisca watu waliweza kuona uwepo wa Mungu katika mkesha huo. Kwa wale wanaomjua Mch. Prisca wataungana na mimi, kwani ni mwimbaji ambaye anajituma katika kazi ya Bwana. Ni Mchungaji ambaye amekulia katika mikono ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tangia akiwa mtoto mdogo sana. Karama yake ya uimbaji ameipata katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ni moja ya waimbaji machachari kwa kazi ya Mungu, ni ni mchungaji ambaye hakika  Mungu anamtumia kwa jia ya tofauti sana. Huduma yake ya uimbaji na uchungaji imebadilisha watu wengi sana Kiroho. Imani za watu zimevuviwa na kuimarika kutokana na uimbaji wa mchungaji huyu na ushuhuda alionao wa kuvumilia kuishi katika mikono ya Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tangia akiwa mdogo sana.

Sasa, tunakukaribisha na wewe katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na siku za katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 1 jioni isipokuwa Jumamosi hatuna ibada. Usafiri ni bure kuanzia nje kidogo ya kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini Dar es Salaam au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” au utasikia watu wakisema kanisania kwa mama Gertrude Rwakatare, ingia humo

 Mch. Prisca

wa pili kutoka kulia ni mtangazaji na mwimbaji wa nyimbo za Injili Victor Aron

 
Mke wa mzee wa kanisa Dr. Mganga


Mch. Stanley Nnko


 Mtoto wa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Rose Rwakatare

 Mch. Noah Lukumay


Mr. & Mrs. Kasembe