RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

01.01.2017: FAMILIA YA KASEMBE YAMSHUKURU BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KWA MALEZI MEMA KIRHO NA KIMWILI KWA KIPINDI CHOTE WAPO HAPO KANISANI

Familia ya Bw. & Bi. Kasembe siku ya Jumapili 01.01.2017 waliweza kumshukuru Mungu kwaajili ya malezi mema waliyopata kutoka kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa kipindi chote walichokuwepo katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini Dar es Salam. Mrs. kasembe alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu asifiwe wapendwa. Kama familia ya Mr. & Mrs. Kasembe, tunamshuku Mungu sana kwa ajili ya Askofu wetu Dkt. Gertrude Rwakatare, tuko hapa leo mahususi kwa jili ya hilo. Nina mshukuru Mungu kwa ajili ya mama kwa upendo wake juu ya waumini wake, amekuwa haumii kabisa kuwepo nyumbani mwa Bwana, akiumwa kidogo yupo haachi kuja kanisani. Uwepo wake umefanyika baraka kwa walio wengi. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare asipoongea neno katika ibada sisi tunapata baraka, tunafurahi na kufarijika. Msione watu wazima kama akina mzee Major Malya wapo kanisani mpaka sasa, ni kwamba bado wanabarikiwa na uwepo wa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kanisani, hata kama siku hiyo hajahubiri ila uwepo wake una nguvu kubwa sana na una uwepo wa Mungu. Tunamshukuru Mungu, kwa ajili ya hilo tu. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa mwaka mzima amekaa hapa kwenye kiti kwaajili yetu, hata akisafiri atahakikisha Jumapili anakuwepo kanisani kwaajili ya kutulea na kuinua imani zetu. Bishop amekuwa anatulea kama watoto wake kimwili na kiroho, hata tukipata matatizo anachukulia matatizo kama yake kwa kutusaidia, amekuwa akitusaidia hata kushinda familia yake ili sisi tuweze kumuona Mungu wetu tutakapotoweka duniani. Anapigwa mikuki na adui zetu ili roho zetu zipone. Tumuombee Bishop wetu kwa wema wake na huruma zake kwetu. Kila mtu sasa aweze kumuombea Bishop wetu katika huduma yake, familia yake na kazi zake.