MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.01.2017: JOYBRINGERS KWAYA NA HAPPY KWAYA ZA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI ZIMEAFANYIKA BARAKA KWA WALIOFIKA IBADANI

Joybringers Kwaya katika ibada ya Kukabidhi Malengo na Mipango yetu iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare tarehe 08.1.2017 imefanyika baraka sana katika wimbo wao wenye nguvu za Mungu. Baadhi ya maneno waliyoimba katika wimbo huu ni kama haya, "Kama si Bwana na Israel aseme sasa,. Macho ya adui yalinisimamia ili kutaka kunisambaratisha lakini kama si Bwana mimi ningekuwa wapi? Shetani ameshindwa na sasa mimi ninaimba. Acheni nimwabudu na nimsifu huyu Mungu wangu kwasababu amenitoa mbali. Mimi ninakusifu Mungu wangu "Halleluya" kwasababu umeniponya na magonjwa, umenipa watoto Bwana". Huu ni ujumbe kwaajili yako wewe. Unaweza sasa kuchukua muda kidogo kwaajili ya kumsifu Mungu wako kwa matendo makuu aliyofanya katika maisha yako. Kuna baadhi ya changamoto ulikuwa unapitia lakini Mungu akakuvusha nazo, na kama bado changamoto zingine  unazo lakini Bwana hajaacha kukuvusha nazo.

Wangapi wamepoteza maisha yao, hawana nyumba, hawana viwanja, hawana magari, hawana watoto, hawana kazi, hawana kibali kazini, hawana elimu, hawana karama kama zako, hawana kipaji kama chako na mambo mengine mema ambayo Bwana amekutendea. Mbona sasa humsifu Mungu wako kwa kuimba na kupaza sauti mbele zake? Mbona umekaa kimia kushuhudia yale aliyokutendea? Mbona huna shukrani mbele za Mungu?  Mbona huna upendo? Umekuwa mtu wa kujivuna, masengenyo, kiburi, mzinzi, huna hekima, husomi Neno la Mungu, muongo, mchawi, mganga wa kienyeji, mshirikina, msengenyaji, matendo mabaya yamekuwa chakula kwako.

Amua sasa kuja kwa Yesu na uache hizo tabia mbaya, kwani hazina utukufu mbele za Mungu, unachafua jina la Mungu wetu. Kanisani unakuja lakini ni muovu, watumishi wa Mungu wanakukumbumbusha kila siku kuacha maovu lakini huachi bado umeshikilia. Ndugu yangu hujui baada ya kifo ni nini kitafuata kwako. Unatakiwa kujiuliza baada ya maisha ya hapa duniani utaenda wapi utakapoiacha dunia hii ghafla pengine kwa ajali au kwa ugonjwa wa ghafla na ukakosa muda wa kuungama. leo hii Mungu anasema uache uovu na umtumikie milele. Mungu akubariki sana.

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" DSM kauanzia saa 9 hadi saa 8 mchana. Usafiri ni Buree Kuanzia Kituo Cha Makumbusho au Mwenge mataa utasikia watu wakisema kwa Mama. Ingia humo utafiki sana.