RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

08.01.2017: MANESA SANGA AWASHA MOTO KATIKA IBADA YA KUKABIDHI MALENGO NA MPIANGO YA MWAKA 2017 KWA MUNGU..

Mwimbaji maarufu sna wa nyimbo za Injili Tanzania aliyetamba kwa wimbo wa "Huyo Ni Chaguo lako" Manesa Sanga, siku ya Jumapili 08.01.2017 aliweza kumtukuza Mungu katika Ibada ya Kukabidi Malengo na Mipango ya Mwaka 2017 iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Mwimbaji huyu alikonga mioyo ya watu kutokana na wimbo wake uliobeba maneno ya kuinua imani za watu na kuwatoa woga kwa yale yalitokea jana na kukabiliana na yale ya kesho.

Kama kawaida yake mwimbaji huyu amekuwa akiongozana na wanae kama dancers wake katika huduma yake ya uimbaji. Watoto wake hao nao ni waimbaji wa nyimbo za Injili.

Tukukaribishe katika ibada ya Jumapili Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ni saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini DSM au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni "B"


Manesa Sanga


 Manesa Sanga



Manesa Sanga



Manesa Sanga