RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

08.01.2017: PRAISE AND WORSHIP TEAM YA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" YAGUSA NAFSI ZA WATU SIKU YA IBADA YA KUKABIDHI MALENGO NA PIPANGO YA MWAKA 2017 KWA MUNGU

Waumini wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" wakiwa na furaha katika ibada ya kukabidhi Malengo na Mipango ya mwaka 2017 siku ya Jumapili 08.01.2017 waliweza kumshukuru Mungu kwa njia ya uimbaji. Mch. Prisca aliweza kuongoza kipindi cha kusifu na kuambudu akiwa na team nzima ya Praise & Worship Team ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Kipindi hiki cha kusifu kilifanyika faraja kwa walio wengi waliokuwa na majaribu na mapito kutokana nyimbo zenye nguvu za Mungu zilizokuwa zikiimbwa. Pia wengine walimsifu Mungu kutokana na yale Mungu aliyowatendea kwa mwaka mzima. Ibada hii ilikuwa na mvuto wa namna yake na uwepo wa Mungu ulitawala. Kanisa zima liliweza kumtumuza Mungu kwa jumuika pamoja na waimbaji hawa.




 Mch. Prisca