MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

08.01.2017: MZEE WA KANISA ANAYEISHI RWANDA KWA SASA ASEMA, TUMUUNGE MKONO BISHOP DR. GERTRUDE KUTUMIZA NDOTO YAKE YA HUDUMA YA MLIMA WA MOTO TANZANIA

Mgeni na mwenyeji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” ambaye kwa sasa ni mkazi nchini Rwanda, siku ya Jumapili 08.01. 2017 aliweza kulisamia kanisani na kumtakia “Happy Birthday” Bishop Dr. Gertrude Rwakatare iliyofanyika Jumapili hii badala ya tarehe 31.12.2016 ambayo ni siku yake “special” aliyozaliwa, alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu asifiwe. Kikubwa hapa tunachotaka kuzungumza ni kuzidi kumtakia mama happy birthday, ni kweli kabisa anastahili kutakiwa heri ya siku yake ya uzaliwa kwa sababu yeye ni mtumishi anawiwa na wengi, hakuna zawadi tunayoweza tukampa zaidi isipokuwa maombi yetu na kumuunga mkono katika maono yake, hii ndio zawadi kubwa kuliko zote. Bishop amekuwa kama Musa, aliyekuwa na zile amri kumi (10) za Mungu, ameinua maono kumi yeye kutoka mlimani kwa Bwana mbinguni. Tumuunge mkono asije akashuka chini kwani amebeba zile amri 10 za Mungu, sasa atampata nani bila kusikiliza maono yake? Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anatupeleka Kanani, tupo jangwani kweli kuna jua, njaa, maumivu lakini hakuna kama Kanani, Biblia inasema, ”hakuna atakayetuongoza zaidi ya Musa”, Mussa wetu wa sasa ni Bishop Dr. Gertrude Rwakatare. Angalia tusije tukaumwa kama wale watu wa jangwani kama tutamuache mbeba maono mama yetu Gertrude, lakini lazima tumuombee sana Bishop kwenye maombi yetu. Hakuna kitu ninachokiomba kila siku kama kumtakia heri Bishop wangu Dr. Gertrude, na kweli toka nimekuja mwezi wa 7/2016 nimeona mabadiliko na maendeleo mengi ya kanisa. Natumaini ninyi wote mlioko hapa mmechangia kwa njia moja ama nyingine kulikarabati kanisa la Mungu la Mlima wa Moto Mikocheni “ B”. Najua faraja ya mama Dr. Gertrude katika Birthday yake kubwa ni kuona kanisa lake linasimama na kuendelea, hakuna zaidi ya hilo vyote ni vyema.Mbarikiwe na Bwana