RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

08.01.2017: WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" WAKABIDHI MALENGO NA MIPANGO YA MWAKA 2017 KWA MUNGU SIKU YA JUMAPILI

Siku ya Jumapili 08.01.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare waumini wa kanisa hilo na wageni waliofika kuabudu siku hiyo waliweza kukabidhi MALENO NA MIPANGO yao ya mwaka 2017 kwa Mungu. Waliweza kuandika mipango yao na malengo yao na kuyakabidhi mikononi mwa Mungu, na watumishi wa Mungu waliweza kuyaombea na baadae kuyachoma moto. Ibada hii ilikuwa ni ibada ya baraka sana.

Tunaamini kuwa Bwana mwenye huruma na upendo kwetu atakwenda kutekeleza yale malengo na mipango tuliyoandika. Mungu wetu tunayemwabudu katika kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B" amekuwa akijibu pale tunapomhitaji, na mwaka huu atakwenda kutusaidia katika malengo yetu tuliyopanga kwa mwaka mzima.

Tunachotakiwa kukifanya kama watoto wa Mungu ni kuzidi kukaa katika uwepo wake na kunyeyekea, kuachana na dhambi na kumtumikia Mungu wetu aliye juu, kuwatii watumishi wa Mungu kwani wao ndio mabalozi wa Mungu na ndio wanatuletea yale wanayoagizwa na Mungu kwaajili ya maisha yetu mafupi ya hapa duniani. Cha msingi zaidi ni kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yetu. Mungu wetu atakwenda kubariki kazi ya mikono yetu ili kufikia yale malengo yetu.

Sasa tukualike katika ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na katikati ya wiki ibada itaanza saa 9 mchana hadi saa 1 jioni. Siku ya Jumapili usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini dar es Salaam au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto au utasikia watu wakisema, kwa mama Gertrude Rwakatare.


Kulia ni Mch. Elizabeth Lucas na Mch. Prisca