RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.12.2016: BISHOP DR. DUNSTAN MABOYA ALIA NA WATU WASIOWAHESHIMU WACHUNGAJI WAO NA KUSHOBOKEA WATUMISHI KUTOKA MAKANISA YA NJE, AKIONGEA KATIKA HITIMISHO LA SHILOH MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


TULIA KWA MCHUNGAJI WAKO MMOJA
Kuna tofauti kati ya Unity na Union sizungumzii union nazungumzia unity. Unity ni sawasawa na unapochukua chupa ya soda inapokuwa imesimama moja peke yake ile ni unity lakini ukiziweka chupa 25 kwa pamoja ile ni union yaani ule mkusanyiko wa kwa pamoja ni union. Pale zikidondoka chupa, kuna zitakazovunjika na zitakazo pona, lakini unity kama moja ikidondoka ni kila kitu kimeharibika. 
Bishop Dr. Dunstan Maboya

Na Yesu hazungumzii union bali anazungumzia unity yaani umoja. Umoja huu utasababisha hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni “B” Moto usizime. Nataka nizungumzie juu ya wahubiri, mara nyingi wahubiri kuwapata kuja kuhubiri kanisani kwako siyo dhambi na wala sio tatizo kuwapata kwasababu wahubiri kama wainjilisti, manabii na mitume ni wengi sana ukifananisha na wachungaji. Kuna manabii wajanja wajanja, wengine wanavitisho wanavyohubiri au kuwatabiria waumni zao.
Kushoto ni Rev. Elias Ndeda kutoka Afrika Kusini

 Kwa sababu watu wanapenda kuwakandamiza watu kutokana na uoga wa vitu fulani ambavyo wanapitia. Lakini kumpata Mchungaji ni kazi ngumu, angekuwa mchungaji wenu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare hana akili, Mungu asingempa dhamana ya kuangalia roho hizi kwa sababu kuna watu wanaongoza watu mia moja lakini wanapigana kila leo, hawaelewani, utasikia huyu kasusa haji kanisani. Lakini Bishop wenu ana hudumia watumaelfu na wametulia tu. Kuna kila kitu, lazima huyu Bishop ni “genius”.


THAMINI CHA NYUMBANI KWAKO
Mara nyingi watu wengi sana hawathamni kitu cha nyumbani kwao. Hautaweza kujua thamani ya kitu mpaka kile kitu kipotee. Watu wamekuwa hawaamini wachungaji wao kwasababu wamewazoea. Mungu amekupa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare mwenye uwezo, nimemwita “genius” nimetumia lugha ya kawaida kwa sababu kuwa mchungaji wa kanisa kama hili kubwa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kunahitaji neema zaidi ya Kimungu kwa sababu kuna kipindi huwezi kuhubiri, 
Kwa mfano unakuta mchungaji kaanda somo linahusu upendo, na kanisani anakuta kuna washirika hawaelewani, na akihubiri upendo kuna mtu atakwazika kwahiyo inabidi aachie kufundisha upendo, pengine anataka kuhubiri uaminifu, kuna mtu anajua njia zake si za kweli katika biashara zake, akitaka kusema jamani tuache wizi anajua kuna mtu ana kesi ya wizi inabidi sasa atumie busara kufundisha juu ya wizi ili asimkwaze muumini wake. 
Haya mambo yamekuwa mengi yanamhalibia mchungaji “message” ya kufundisha, sasa hapo inabidi atumie uzoefu wa kichungaji na siyo kuhubiri. Kuhubiri mtu yeyote anaweza akahubiri. Watu wengi wanaumiza kichwa lakini mchungaji anakufanyia maombi kwa sababu yeye haangalii “issue” uliyonayo anaangalia mbegu iliyopo ndani mwako. Tunamuona Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anakemea makosa na hafugi makosa kwasababu anaangalia mbegu iliyo ndani yako. Uchungaji siyo kuhubiri usije ukamlinganisha mchungaji wako na mwinjilisti.
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare


KWANINI HUPENDI CHA NYUMBANI KWAKO?
Watu hawapendi kuthamini cha nyumbani kwao, hawathamini wachungaji wao, ila akija mwinjilisti kutoka kanisa jingine utaona wanavyoshobokea. Mwinjilisti anaweza akawa na mstari mmoja tu wa kuhubiri siku hiyo na akahubiri na mengine akaongezea na ya kwake na akakusanya sadaka akaendelea mbele.
 Lakini hawezi kukulea kwasababu yeye ni mtu wa kupita, lakini mchungaji wako ni lazima awe na “message” nyingi. Kuna wakati unafika mchungani wako hana ujumbe anakaa analia mwenyewe, anajiuliza nitafanya nini leo kwa waumini wangu? Nitafundisha nini?, Kwa sababu kila ujumbe anaotaka kuutoa unaumiza mtu. 
Ndani ya kanisa kuna mwingine ana kesi police, mwingine ana matatizo ya talaka, mwingine maisha ndio yanambana, mwingine kodi ya nyumba, mwingine hana chakula, mwingine anawaza watoto. Mchungaji anaanza kuwaza hivi nikihubiri hili, Je, huyu mwingine atanielewa? Ninataka kuwapa hili neno “Mkamheshimu mchungaji wenu”. Hebu angalia mko wa ngapi hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”, na mchungaji wenu anavumilia managpi? Nataka kukuambia kuwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ni “genius”. 
Ninajua maumivu ya kuachwa, siku moja nilikuwa na mtu ambaye alikuwa “very close” na mimi nikawa na mwamili ndio kila kitu kwangu lakini akataka kuniua siyo kwa kuniwekea sumu wala bangi!! Ila alinitoroka bila taarifa alafu akawa upande mwingine “very close” Amekuwa na mimi kwa muda wa miaka mitano, sita ananiacha mwenyewe, niliumia sana. Kaa na mchungaji wako, utainuliwa zaidi.



KWANINI UMTESE MCHUNAGAJI WAKO?
Baadhi ya waumini wamekuwa wakiwatesa sana wachungaji wao kwa kutotii yale wanayoambiwa na Mungu kupitia vinywa vyao, na ukifanya uchunguzi utaona sababu kubwa ni kwamba wamewazoea. Mimi baada ya kuumizwa na muumini wangu niliyekaa naye miaka sita aliyekuwa ”very close” kwangu aliponikimbia nikaanza kuhema mwenyewe, nakunywa panadol, huku nawaza mwingine nitamuinua kwa kiasi gani kwa miaka mingapi ili niwe salama? 
Wachungaji wana mambo mengi sana wanapitia katika huduma zao ila mimi ninawapa tu ushauri tena kwa herufi kubwa MTIINI MCHUNGAJI WENU, mnaweza mkawa na wachungaji thelathini lakini mbeba maono ni mmoja tu, unaweza ukawa na mtu ambaye amaomba mpaka anatetemeka lakini mbeba maono ni mmoja tu. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare unaweza ukashangaa kuna kipindi watu unao waamini wakakkumbia na ukaumia sana, lakini kwasababu wewe ni mchungaji unasamehe na kuwaombea. 
Kuna siku moja niliumizwa sana kuna vijana wangu wawili ambao nimewainua mwenyewe wapo kanisani mi nahubiri wao wanatia “story” zingine, wanasema, “Anahubiri nani? Maboya, aah tusimisikilize tumemzoea huyo!”. Lile neno lilipokuja kwangu nilitamani sijui nimpe jibu gani? Nikasema, “Mungu naomba msamehe huyu mtu”, Halafu bado unakula nae, yaani nilitamani nimchape makofi . Siku moja alipolazwa hospitalini nilitamani nimkumbushe, Mungu akasema msamehe. Tuwaheshimu na kuwatii wachungaji wanamchango mkubwa kwetu.

Katikati ni Mch. Noah Lukumay

KUNA FAIDA KUBWA YA KUMHESHIMUMCHUNGAJI WAKO
Mtakavyo muheshimu mchungaji wenu kuna neema mtaipata na siyo tu mchungaji wako umlinganishe na mchungaji mwingine hapana, maana kwenye wachungaji kuna “Under Probation Pastors”, halafu kuna wale “Comfirmed Pastors” na mwisho kuna “Covenant Pastors”. Sasa hawa “Covenant Pastors” ambao wao wanatumwa na Mungu akicheka tu wewe unabarikiwa, akizungumza lolote unabarikiwa, akirukaruka unabarikiwa. 

Mchungaji wenu mama Gertrude Rwakatare alishaondoka kwenye “Under Probation Pastors”, “Comfirmed Pastors” sasa anatembea kwenye “Covenant Pastors”. Siku ukimuona anahubiri akakuachia ukahubiri, usije ukaanza kuinua mabega na kujiona wewe kidume katika madhabahu. Kuna siku moja nilikuwa nimeenda sehemu halafu binti yangu alipokuja akahubiri mpaka watu wakasema, “Roho wa Mungu ameingia kwa baba yake halafu amehamia kwa mtoto wake”. 
Waliokuwa wanazungumza ni watu wazima, mimi nikaliweka moyoni. Sasa kuna siku wakawa na “issue” ya ndoa, nikasema usiwe na wasiwasi wewe ni mwanangu ukweli ninaweza kushindwa kuruka, lakini kunauzoefu ninao, nyani hucheza hukwepa mishare mingina hawezi kukuacha bure atakupigani. Nikamwambia mwanangu ngoma hiyo hapo yakufungisha ndoa. Waliposikia mwanangu ndiye atakayehusikia wakagoma wakawa wanahitaji nikafungishe ndoa. Ninachotaka kusema ni kwamba, mchungaji wako ni mchungaji wako tu, mheshimuni sana, amebeba mizigo yenu.



SIO KILA MTU ANAFURAHIA HUDUMA YAKO
Mungu amempa kila mtu dhamana kubwa mno ndani yake ambayo inaweza kusaidia maisha ya mwingine yakaendelea kuwa bora zaidi. Mungu amewapa wengine kuwa wachungaji. Nataka niwaambie kuwa kazi ya hii ya uchungaji siyo kila mtu anaifurahia na ni “nature” ya watu hawapendani. Utakuta mchungaji huyu anachukia huduma ya mchungaji mwenzake, watu wanaonea wivu sana hasa katika suala na uwingi wa waumini. Inafika “point” wanazushia maneno ili waumini wawachukie wachungaji wao na kuhama kanisa. 
Ikiwa wachungaji wanaume kwenye huduma tunaoneana wivu, sasa vipi je mwanamke akiwa anaongoza kundi kubwa kama Bishop Dr. Gertrude Rwakatare? Watu wanaumia sana wanapoona mwanamke anakuwa na kundi kubwa la waumini. Mashambulizi yote anayopata mbeba maono, anayapata kwa ajili ya urithi wenu, kwahiyo ni lazima usimame nae kwenye hali zote na ukifanya hivyo kila jambo utakalofanya utaona unabarikiwa, utaona unainuliwa unafanyiwa vitu vya tofauti. 
Watu hawajui kuwa unapomsukuma chura unamsaidia kusogea mbele na kuyafikia malengo yake, kwahiyo unapompiga vijembe mchungaji wako ndio unasababisha watu kumpenda na Mungu kumfungulia milango ya mafanikio. Kuna usemi unasema, “Aliyenacho ataongezewa asiye nacho kile kidogo atanyang’anywa”. Nachokuomba ni sana na kutii maagizo ya wachungaji wako, kuwaheshimu na kuwapenda kwani wao wamechanguliwa na Mungu kuwa mabalozi wake hapa duniani ili uokolewe na ufike mbinguni kwa Baba