RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

15.01.2017: BISHOP DR.GERTRUDE RWAKATARE MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" : KUGAWA MBEGU


Katika ibada ya kukabidhi vitendea kazi vyetu na kuombea mikono yetu siku ya Jumapili 15.01.2017, Bishop Dr. Gertrude aliweza kugawa mbegu ya fedha kwa watu wote waliofika katika ibada hiyo Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mbegu hii ilikuwa kwaajili ya kuwaondoa watu kutoka katika umaskini na kuelekea katika utajiri. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na jopo la wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliweza kuziombea mbegu hizo.

Bishop aliweza kuwagawia wazee wa kanisa na baadae kwa waumini na wageni wote waliofika kanisani kumtukuza Mungu wetu. Kanisa hili limekuwa likifanya zoezi hili la ugawaji wa mbegu na watu wamekuwa wakifanikiwa katika kazi zao na ofisi zao. Mungu ni mwema sana kwani amekuwa mwaminifu sana kwa waliowaaminifu kwake. Na kupitia mbegu hii iliyotolewa Jumapili tunasubiri majibu kutoka kwa Bwana, kwani imani yetu ni kwamba Bwana amesikia na amepokea maombi yaliyoombwa na watumishi wa MUNGU.

Sasa nikuombea Jumapili hii usikose katika ibada itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu ana kitu cha kufanya kwako siku hii maalum. Usafiri ni bure kabisa kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini dar es salaam au Mwenge kwenye mataa, utayaona magari yetu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" au utasikia watu wakisema kwa mama Gertrude Rwakatare, ingia huo, na baada ya ibada utarudishwa kituo bila ya nauli