MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

31.12.2016: ANISETH BUTATI NA KASAKI SELEMANI WAKONGA MIOYO YA WATU KATIKA MKESHA WA KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016 (CROSSOVER) - MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa jinsi anavyowatumia waimbaji hawa (Aniset Butati na Kasaki Selemani) katika huduma ya Mlima wa Moto Mikocheni "B".
Katika mkesha wa CrossOver 2016 wa kukaribisha mwaka mpya 2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", tumeshuhudia jinsi Mungu alivyowatumia waimbaji hawa.

Tulibarikiwa sana na huduma yao na tuliona uwepo wa Mungu ukitanda katika kanisa hili la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Waimbaji hawa wanajituma sana kwa kazi ya Mungu na wamefanyika baraka kubwa sana katika kanisa hili. Kila wanapokuwepo madhabahuni kwaajili ya kumtumikia Mungu tunaona nguvu za Mungu zikigusa maisha ya watu.

Kuna baadhi ya watu wanakuja kanisani wakiwa na "stress" za kimaisha au stress za magonjwa, lakini wanapokutana na waimbaji hawa wanapata faraja ya mioyo yao kutokana na ujumbe uliomo katika nyimbo za hawa waimbaji.

Tuna kila sababu ya kuwaombea ili wazidi kufanya kazi ya Mungu, kwani wao bado ni vijana sana na wana nguvu kubwa kwaajili ya kujenga ufalme wa Mungu.

Tunakukaribisha na wewe katika ibada ya Jumapili hii katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu na akubariki sana.