RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

31.12.2016: MAMIA YA WATU WAOKOKA KATIKA MKESHA WA KUKARIBISHA MWAKA 2017 (CROSSOVER) KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" - DAR

Tuna kila sababu ya kusema Asante Yesu. Tumeona Yesu akiokoa watu siku ya mkesha wa kukaribisha mwaka 2017 (Crossover) katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
watu wengi sana walijitokeza kumpokea bwana kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao na pia waliapa kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuwa waumini wa kuduma.
Mch. Noah Lukumay pamoja na jopo la wachungaji waliweza kuwaombea na kuwaongoza sala ya toba na baada ya hapo walipewa fomu maalum ya kujiunga na kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
Baada ya mkesha kumalizika kanisa limepanga siku maalum kwaajili ya kuwabatiza kwa maji mengi.
Tunazidi kusema asante Jehovah kwa upendo wako huo, maana ameona watoto wake wanateseka na taabu za dunia na akaamua kuwaokoa.
Ni zamu yako sasa kuja kwa Yesu ili aweze kugusa maisha yako. yawezekana unasumbuliwa na madeni, magonjwa, umaskini, kukosa ada, kukosa kodi ya nyumba, laana, mikosi, roho za kukataliwa, unalogwa, wachawi wanakutumikisha, haupandishwi cheo yaani kila mahali ni mateso. Leo Bwana anakuita njoo akusaidie hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B".
Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia nje kidogo ya kituo cha mabasi cha Makumbusho -Dar au Mwenge, utaona watu wakisema kanisa kwa Mama Rwakatare au Mwenge kwenye mataa. Mungu akubariki sana

 Mch. Noah Lukumay