MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

31.12.2016: ZAKAYO AFANYA MAMBO YA AJABU YA KUMPENDEZA MUNGU KATIKA MKESHA WA KUKARIBISHA MWAKA 2017 (CROSSOVER) MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"


Mungu azidi kumbariki mtumishi wake Zakayo, amefanyika baraka katika mkesha wa kukaribisha mwaka 2017 kat0ika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumamosi 31.12.2016. Tulibarikiwa sana na uimbaji wake na anavyojituma katika kucheza. Tuliona uwepo wa Mungu juu yetu ukituzunguka. Tunakuombea sana mtumishi wa Mungu uzidi kusonga mbele kwa kazi ya Bwana, maana Bwana amekuchagua ukiwa bado kijana kufanya kazi yake, Kuna watu wengine wameshindwa kufanya huduma unayofanya na wanatamani kufanya lakini wanashindwa ila wewe Mungu amekupa nguvu na karama ya uimbaji.

Sasa, nikukaribishe wewe mdau wa akaunti yetu ya fb kufika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ibada itaanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa hapa DSM. Pia tuna ibada katikati ya wiki kuanzia saa 9 mchana hadi saa 1 jioni, kwa siku hizo usafiri unajitegemea. Mungu akubariki sana.