RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

ASKOFU MOKIWA: MIMI NI ASKOFU HALALI WA JIMBO LA DAR


ASKOFU Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam Dkt. Valentine Mokiwa amesema kuwa yeye anatambua bado ni ndiye askofu wa Dar na hakuna mtu wa kumfukuza bali mtu wa kumfuta kazi ni Sinodi ya Dar, Kanisa la Anglikana lina kanuni na taratibu zake wala sio askofu mkuu au askofu mwingine yeyote wa kanisa la Anglikana Tanzania.


Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam alipozungumza na vyombo vya habari baada ya tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi yake yanayodaiwa kufunguliwa na walei 32 (waumini) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam yakiwemo ya ufisadi wa mali za kanisa.


Anayedaiwa kuvuliwa uaskofu Dkt. Valentine Mokiwa akizungumza na wanahabari.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dkt. Jacob Chimeledya ndiye anayedaiwa kumvua uaskofu Mkuu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.

Dkt. Mokiwa amesema kuwa tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake ni za kumchafua na kulenga kumchonganisha dhidi ya waumini wake na wanaofanya hivyo ni wale waliokiuka miiko ya kanisa akawavua vyeo, huku akiwataja kuwa ni Mchungaji John Mhina, mchungaji Johnson Chinyong’ole wa kanisa la Newala na Paul Mtweve aliyemtaja kuwa alikuwa katibu wa uinjilisti Dayosisi ya Magomeni.

Alisema kuwa hao ndio wavunjifu wa amani katika dayosisi hiyo ndio maana akaamua kuwatimua na hivi sasa wamerudi kivingine ndio hao hao ambao wamesababisha mgogoro huu unaojitokeza hivi sasa.


Akisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.Hawapo pichani.


Dk. Mokiwa alisema kuwa alishangazwa, askofu mkuu Dk. Chimeledya na ujumbe wake kuhudhuria kikao cha hivi karibuni cha Halmashauri ya kudumu ya dayosisi ya Dar es Salaam na kutangaza uamuzi wa kumvua uaskofu tena kukiwa na ulinzi wa polisi kinyume na utaratibu wa kanisa kuja na askali kanisani.

“Mwenye mamlaka ya kunifukuza kazi ni yule aliyeniajiri, na mwajiri wangu ni Sinodi ya Dar es Salaam na wote wanasambaza habari hizi za uchochezi ni wale niliowavulisha madaraka ya kuwa viongozi. alisema


Mwandishi wa mtandao huu, Denis Mtima akimpa tuhuma zake mchungaji, John Mhina wa kainisa la magomeni zilizotolewa na Askofu Mokiwa.


Alisema waraka ambao umesambazwa na askofu mkuu wa Tanzania haujapitia kwenye halmashauri ya kudumu ya dayosisi ili kupata baraka zake na wala hauna baraka kutoka kwa sinodi ya dayosisi jambo ambalo linaufanya waraka huo ukose sifa za kutekelezeka.

“Ninachowaambia ndugu waandishi wa habari mlifanya makosa kusambaza taarifa bila kuninukuu mimi ili muweze kuandika kilicho bora tofauti na kuandika vitu visivyokuwa vya kweli na askofu wa dayosisi ya Dar es Salaam bado ni mimi, hatuzitambui barua zilizosomwa katika baadhi ya makanisa,” alisema

Askofu Mokiwa alisema baada ya kikao kilichofanyika hivi karibuni katika kanisa la ilala Dar na kuhudhuriwa na viongozi wakuu huku wakisoma walaka wa kumvua cheo hicho mbele ya halmashauri, lakini maamuzi hayo yaligomewa na wajumbe wa halmashauri ya Dayosisi ya Dar es Salaam.


Mahojiano yakiendelea.aliyeko kulia ni Paul Mtweve katibu wa uinjilisti


“Ule waraka tuliupitia na kubaini kuwa hauna baraza za nyumba ya maakofu, wala hauna baraka za halmashauri ya kudumu na Sinodi ya dayosisi,” alisema na kuongeza kuwa maamuzi ya kumvua uaskofu Dk Mokiwa yamefanywa na askofu mkuu wa Tanzania kwa kushinikizwa na watu wachache aliowavua vyeo na sio vikao vya kanisa.

Lakini alipoulizwa askofu mokiwa swali na waandishi wa habari kuhusu kudaiwa kutelekeza Nyumba iliyopo Osyterbay na nyingine iliyopo Upanga jijini Dar alisema kuwa nyumba hizo siyo za kwake bali ni mali ya kanisa na sio zimetelekezwa bali zipo katika hatua ya ujenzi wa nyumba za kisasa.

Risasi liliwatafuta baadhi ya watuhumiwa waliolalamikiwa na Mokiwa kwa kusababisha mgogoro huo ambao ni Mchungaji John Muhina wa Magomeni na Paul Mtweve ambae alikuwa katibu wa Uinjiristi ambao kwa upande wao kwanza walikataa kumtambua Mokiwa kama askofu tena kwani kasha vuliwa wazifa huo.

“ Sisi ni viongozi halali wa kanisa la Anglikana Magomeni Mokiwa alitusimamisha kipindi cha uongozi wake lakini tukaamua kukata rufaa sehemu husika tukashinda.

Askofu hana uwezo wa kutuondolea uchungaji, anauwezo wa kutuvua uaskofu laikini kikatiba tuliamua kwenda kukata rufaa katika mamlaka ya juu ambayo yeye hana mamlka nayo ambayo ni kwa askofu Mkuu na alilidhia rufaa yetu tukashinda,’’ alisema na kuongeza.

“Mbona yeye analalamika kuondolewa uaskofu, wakati sisi anatusimamisha alisema amefanya mabadiliko ya kawaida tu,tukakubali laikini tukaenda kukata rufaa kwenye mamlka za juu tunaona asiweke visingizio vyovyote dhidi yetu bali akubali uamuzi uliotolewa na Askofu wetu mkuu.

BONYEZA HAPA KUONA VIDEO

NA DENIS MTIMA/GPL