RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

“CHANJO YA UGONJWA WA PEPOPUNDA IPO YA KUTOSHA” – WIZARA YA AFYA

Baada ya kuripotiwa taarifa kwamba kuna uhaba wa kinga za ugonjwa wa Pepopunda kwenye Hospitali za Dar es salaam, Leo January 2, 2017 Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto imetoa ufafanuzi kuhusu chanjo hiyo na kueleza kuwa ipo akiba ya kutosha tofauti na ilivyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima leo Jumatatu ya tarehe 02/01/2017.

Wizara ya Afya imesema kuwa habari iliyotolewa na gazeti hili sio sahihi, na hata majina ya watu waliohojiwa kuhusu kuadimika kwa chanjo hiyo hawapo wizarani, na wengine wapo masomoni, hii ni taarifa yazamani sana kimsingi imepitwa na wakati ambayo haikupaswa kutolewa kania wahariri wa habari wangekuwa makini katika kufanyia kazi taarifa hii.

Kwenye taarifa hiyo ametajwa Daktari kiongozi wa hospitali ya Amana, Stanley Dinagi, ambaye sasa hivi hayupo nchini, yupo masomoni. Pia katajwa Mganga mkuu wa serikali Donald Mmbando ambaye hayupo katika wadhifa huo sasa imepita takribani miaka mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya, Nsachris B. Mwamaja imefafanua uwepo kinga hiyo katika wilaya kuu tatu za Dar es salaam.

Mkoa wa Dar Es Salaam una chanjo za Pepopunda zakutosha katika manispaa zake zote na umesambaza mgao wake kama ifuatavyo,
ILALA – Dozi 35,300 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016 na mahitaji yao kwa mwezi Dozi 7,110.
TEMEKE – Dozi 33,000 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni Dozi 7,620.
KINONDONI – Dozi 11,000 zilisambazwa Tarehe 07/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni dozi 9,210.

“Kwa hivi sasa hakuna upungufu wowote wa chanjo ya pepopunda nchini, Tuna jumla ya dozi 599,000 katika bohari ya taifa, na tunatarajia kupokea shehena nyingine ya dozi 1,200,000 wakati wowote ili kuhakikisha kwamba hatuna uhaba wa chanjo hii.” – Mwamaja