MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

DAVID ROBERT MWAMSOJO: MUNGU AKUKUTANISHE NA WATU SAHIHI MWAKA HUU.

David Robert Mwamsojo

Upo umuhimu mkubwa sanaa kati ya maisha na watu unaohusiana nao. Level ya maisha ulionayo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya watu unaohusiana nao.


Mahusiano yapo katika level tofauti wapo unahusiana nao kwa udugu wa damu, marafiki uliojichagulia, majirani uliokuwa nao, unaokutana nao kazi, biasharani,kwenye nyumba za ibada, shuleni na maeneo kama hayo.

Yapo mahusiano katika level nyingine mke, mume wazazi watoto, na ndugu wa karibu.

Aina hizo zoote zimekufanya ulivyo. Kuna watu ukuchangu imetokea by nature kwa mfano huchagui dada au kaka wala wazazi, inatokea tu wewe ni wa hiyo familia. Pia majirani unapojenga au wazazi wako walipojenga mlijikuta mko na majirani furani.

Lakini kupevuka kimwili na kiroho pia ni kuwa na uwezo wa kutambua tija ya mahusiano na unaohusiana nao. Je wanachangiaje mafanikio yako kiroho na kimwili? Haya ni maswali anayojiuliza mtu mzima tu aliepevuka kiakili sio kimaumbile.

Huwezi kung'ang'ana na watu ambao hawana athari njema kwenye maisha yako ukategemea kuwa na mabadiriko. Sijui sana kwanini MUNGU anamwambia Abraham ondoka kwenye nchi ya baba yako? Ukisoma katika kitabu cha mwanzo unaona wazazi wake walikuwa wanaabudu sanamu.

Hapa nayaona mahusiano mengine mazingira nchi ya baba yako haya ni mazingira. Mazingira yanaweza pia yakaadhiri mtazamo wako kwa mfano nilikuwa kwetu Mbeya nilijua Dunia yote imezungukwa na milima kama mji wa Mbeya lakini nilipofika Dar Es salaam nikaona sio kweli. Anyway siko kuongelea mazingira leo.

Baada ya kujitathimini juu ya watu unaohusiana nao ni maombi yangu MUNGU ayafungue macho yako ya roho uone umuhimu wa mausiano na Roho Mtakatifu akuongoze jinsi ya kutoka hapo.

Usivunje mahusiano na watu, marafiki kusudi ilo ni jambo baya ambalo laweza kusababisha maumivu kwa wahusika. Unaanzaje kumwambia mtu kuanzia leo wewe si rafiki yangu it's hard!

Jambo la kufanya muombe Mungu akubadirishe wewe ufanane na mtu anaeyaelekea mafanikio taratibu utaanza kubadirika na wavivu wataanza kujiengua kama ulikuwa mnywaji wa pombe walevi wataanza kutitenga nawe, kama ulikuwa na watu mnaovizia totoz pamoja wataanza kujiengua, waleta majungu mapema wataanza kukukwepa.

Maana yale yoote yaliokuwa yanawaunganisha hunayo tena umeanza kuishi maisha ya kimakusudi ukipangilia mambo, ukiukomboa wakati, mtazamo wako umebadirika complete. Watasema analinga anajifanya yuko juu siku hizi na maneno mengi kama hayo .

Ni maombi yangu Mungu akukutanishe na watu sahihi ambao hawatavumilia kukuona unapotea wanyamaze, watakao kuonyesha fursa ya kuongeza kipato, watakao kujenga kiroho watakaokuwa washauri wako kiuchumi, maisha ya ndoa, malezi ya watoto na mengi mazuri wakushauri