MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

KADA WA CCM BUCHOSA AWASHIKA MKONO VIJANA WA KATA YA KATWE.


Awali kada huyo wa CCM aliwakabidhi mabati mia moja vijana wa kijiji cha Mwagika ili waweze kuwekeza kwenye mradi wa kuwaingizia kipato.

NA:- ZEPHANIA MANDIA.
Wakazi wa kata ya katwe halmashauri ya wilaya Buchosa mkoani Mwanza wametakiwa kutatua changamoto zinazokikabili kituo cha afya cha mwangika ikiwemo ufinyu wa wodi ya uzazi pamoja jengo la upasuaji badala ya kuisubiri serikali.

Wito huo umetolewa na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ESTON KASIKA ambaye ameahidi kuwaunga mkono wananchi hao kwa kutoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mbao, misumari pamoja na mabati mia moja huku akiwataka kufyatua matofali,kusomba mawe na mchanga.

Kituo cha afya cha mwangika halmashauri ya wilaya buchosa mkoani Mwanza kinakabiliwa na ufinyu wa wodi ya uzazi pamoja na ukosefu wa huduma ya upasuaji na hivyo kuzorotesha utoaji wa huduma kwa akinamama wajawazito.

Wakizungumza na vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kata ya Katwe wameiomba serikali kuboresha utoaji wa huduma ya uzazi katika kituo hicho ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto vinavyotokea wakati wa kujifungua.

Kada wa chama chamapinduzi (CCM) ESTON KASIKA akiteta na wananchi wenzake.

Kwaya ya AIC Nyahunge.

Timu ya soka wakazi wa kata ya Katwe imepokea vifaa vya michezo ikiwemo mipira.


Kilio cha wakazi hao kimemgusa kada wa chama chamapinduzi(CCM)na mkazi wa kijiji cha mwangika ESTON KASIKA ambaye amewataka wananchi kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho cha afya.