RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KANISA LA POOL OF SLOAM LATOA MSAADA WA MATAILI MATANO KWA KITUO CHA POLISI NGURUKA MKOANI KIGOMA

Kupitia jitihada za zinazofanywa na Asasi,taasisi,makampuni na watu binafsi,kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa lengo la kukamilisha huduma mbalimbali kwa Umma ,Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma amepokea jumla ya mataili 05 yenye thamani ya shilingi millioni mbili na laki nane ili kuboresha gari la polisi la kituo cha Nguruka kata ya Nguruka wilayani Uvinza.
Akipokea mataili hayo yaliyotolewa na kanisa la Pool of Sloam,kwa niaba ya Naibu kamishina wa polisi Mkoani Kigoma,Ferdinand Mtui,mkuu wa polisi wilaya ya Uvinza Amedeus Malenge amesema kuwa kitendo kilichofanywa na kanisa hilo kitasaidia kuifikia jamii kwa wakati hasa wahalifu.

Kwa upande wake Kuhani UFAHAMU HAKIKAZI ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya uhitaji wa mataili hayo,kanisa limechukua hatua hiyo kwa kuwa kanisa na Serikali hufanya kazi pamoja katika kukamilisha huduma za kijamii.
Matairi hayo yaliyokabidhiwa katika kituo hicho cha polisi Nguruka.

Aidha kuhani.HAKIKAZI ameongeza kuwa ,kupitia mahitaji ya kuboreshwa kituo cha polisi kilichopo kijijini humo,amesema kuwa amelichukua na atalifikisha kwa uongozi wa kanisa ili kuona namna linavyoweza kufanyiwa ufumbuzi wa kuboresha kituo hicho.

Nao viongozi wa kijijini humo akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha nguruka Bw.Mosha Mohamed na mwenyekiti wa kitongoji cha nguruka kusini Hamis Kiliza,wamesema kuwa kwa kuwa huduma ya polisi inauhitaji mkubwa kwa jamii,mataili hayo yatasaidia kupunguza uhalifu kwa kuwa kazi sasa zitafanyika kwa wakati huku wakiomba kuboreshwa tena kwa kituo hicho cha polisi kwa kuwa sasa hakitoshi kutoa huduma kulingana na wingi wa wahalifu wanaowekwa ndani ya kituo hicho.

Kuhani Ufahamu akipeana mkona na Mkuu wa Polisi wilaya ya Uvinza mara baada ya kumkabidhi mataili hayo.
Wakijadili.jambo nje ya kituo hicho cha polisi Nguruka