RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MTOTO ADAIWA KUMUUWA BABA YAKE MZAZI KISHA KUCHIMBA SHIMO LA KUTAKA KUMZIKIA,SONGEA

Mwenye t shirt ya damu ya mzee ni Pius Malindisa ambaye ni mdogo wake marehe

mu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio lilivyotokea katika kijiji hicho.Nyumbani kwa kwa marehemu Atanas Patrick watu wakiwa wamejitokeza kwa ajili ya kwenda kumstili.

Na Amon Mtega
JESHI la polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) makazi wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Atanasi Malindisa (70) kwa kumpiga na kitu chenye ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto kisha kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzikia baba huyo.
Akizungumza na Ruvuma TV katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Piusi Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu majira ya 1.30 kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrck Malindisa .
Piusi alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu huyo alitoa taarifa kwa wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Atanasi Malindisa ameuwawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.
Alisema kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa polisi kisha mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuuhifadhi Hospital ya mkoa Ruvuma [HOMSO] kwa uchunguzi huku jeshi la polisi likimshikilia mtoto wa marehemu kwa mahojiano zaidi.
Alifafanu kuwa polisi wakiwa bado kwenye nyumba hiyo walibaini kuwa kwenye moja ya chumba ambacho hakijaezekwa kulichimbwa shimo linaloendana na vipimo vya marehemu ambalo lilihisiwa kuwa alitaka amfukie humo ili watu wasijue kwa kuwa kwenye nyumba hiyo walikuwa wakiishi wawili.
“Uchimbaji wa shimo hilo lenye mithiri ya kaburi lilimshinda kisha akamua kulifukia na kuchukua hatua ya kuja kutoa taarifa kwetu wanandugu kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo ambayo inadaiwa alikuwa akilia nalo kumbe sivyo bali kapigwa na kitu kichwani”alisema Ndugu wa marehemu.
Kwa upande wake jirani wa nyumba hiyo ambaye hakutaka kulitaja jina lake alisema kuwa maisha ya marehemu na mtoto wake walikuwa wakipigana mara kwa mara hasa kwa kutumia silaha na majirani walikuwa hawapo karibu nao kutokana na tabia hizo.
Vituko vya tawala kwenye makaburi ya Namanyigu wakati wa uchimbaji wa kaburi la kumzikia marehemu Atanasi Malindisa ambako mtandao huu umeshuhudiwa vijana walitaka kugomea kuchimba kaburi hilo kwa madai kuwa familia hiyo ilikuwa haijihusishi kwenye matatizo ya majirani.
Baadhi ya wazee waliwasii vijana hao kwa kuwaomba wasilipe ubaya kwa ubaya cha msingi wafanikishe kumuhifadhi marehemu kwa kuwa marehemu hayupo duniani hivyo ni vema wakasamehe na kumuachia Mungu.
Katika usafirisaji wa mwili huo kutoka katika Hospital ulikohifadhiwa baada ya magari ya maeneo hayo kutokuonyesha nia ya kutoa msaada gari la Mbunge wa jimbo la Songea mjini Leonidas Gama ambalo alilitoa kwa wananchi kwaajili ya matatizo mbalimbali la okoa jahazi kwa kuubeba mwili wa marehemu huyo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na kumshikilia mtuhumiwa Patrick Malindisa mtoto wa marehemu na kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi likiwemo shimo lililokutwa.