RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NAIBU WAZIRI JAFFO AAGIZA KUUNDWA TUME YA KUCHUNGUZA MAMILIONI YA FEDHA YALIY0TOLEWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MKURANGA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kuunda Tume ya kuchunguza upotevu wa fedha za dawa katika Hospitali ya Mkuranga, Mfumo wa ukusanyasaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi. 

Jaffo ametoa agizo hilo wakati alipokutana na watendaji wa Halmashauri ya Mkuranga mapema jana, amesema serikali ilitoa sh. milioni 258 kwa ajili ukarabati wa Hospitali kati ya hizo Sh. milioni 86 ni za kununulia dawa, lakini dawa zilizonunuliwa katika Hospitali hiyo ni za sh. Milioni 22 na fedha iliyobaki haina majibu 

Amsema wananchi wanahitaji dawa kutokana na fedha wanayochangia katika huduma ya afya, kukosa dawa kwao suala ambalo sio matarajio yao. 
Jaffo amesema ukusanyaji mapato katika hospitali ya Mkuranga sio mzuri kutokana na kutumia mfumo wa makaratasi ikilinganishwa na sehemu nyingine kutokana na kutumia mashine za Kieletroniki. 

Amesema Hospitali ya Mkuranga inakusanya mapato ya sh. Milioni 2.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana sh. milioni 2.1 ambapo ongezeko lake ni sh. 600, 000 wakati Hospitali zingine zinakusanya zaidi ya sh. milioni 20. 

Mwitikio wa kufika kwa Naibu Waziri Jaffo kulitokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ambaye alifanya ziara katika vijiji 90 na malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa dawa katika Hospiali ya Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

Hata hivyo, Jaffo ametoa agizo la Kisima cha Mwarusembe ndani ya siku tatu awe amepata majibu ya kuridhisha kutokana wananchi kukosa maji kwa muda mrefu. Nae Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema wananchi wanaweza kuondokana na tatizo la kukosa dawa kutokakana watendaji kufuata taratibu za uombaji.
.Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Mkuranga mapema jana alipofanya ziara katika Wilaya hiyo .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akipata maelezo ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega juu ya wananchi kulalamikia upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkuranga katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Muonekano wa Wodi ya Wazazi Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo alifanya ziara mapema jana .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akielezwa na mgonjwa, Emiliana shila aliyefika katika Hospitali Mkuranga akiwa na vifaa Tiba na Dawa alizoambiwa akanunue nje .
Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mapema jana alipofanya ziara katika Wilaya hiyo.