RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

NJIA 10 MUHIMU UNAZOTAKIWA KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUWA MILLIONEA.


1. Ongeza Kipato Chako
Katika ulimwengu wa sasa, kiuchumi ni vigumu kutunza pesa kwa kiwango cha kipato kidogo mpaka kuufikia umillionea. Hatua ya kwanza ni kuongeza kipato chako bila kukoma, kutoka katika chanzo au vyanzo mbalimbali vya mapato yako. Kama kipato chako ni Tshs 300,000 kwa mwezi fanya jitiahada binafsi za kuongeza kutoka la Tshs 300,000 kwenda Tshs 10,000,000 na zaidi kwa mwezi. Anzakufanya jitihada za kuongeza mapato yako kutoka katika biashara au ajira uliyopo sasa.

2. Acha matumizi mabaya ya pesa
Acha matumizi mabaya ya pesa hasa kwa matumizi yasiyo ya lazima, hakuna haja ya kununua vito vya thamani au mavazi wakati hata haujaikuza biashara yako au kuifikisha sememu inapostahili.


3. Tunza na Kuwekeza
Usitunze pesa kwa ufahari. Tunza pesa ili zikusaidie katika shughuli za uwekezaji. Anza kutunza pesa katika akaunti maalum ya akiba, pesa hiyo isitumike hata kwa matukio ya dharula. Hii itakusaidia kuendeleza utekelezaji wa hatu yetu ya wali ya kuongeza mapato yako.

4. Epuka mikopo isiyokuwa na faida
Jiwekee sheria ya kutochukua mikopo isiyoweza kukuongezea pato lako. Watu matajiri hutumia mikopo kujinufaisha kwa kuwekeza sehemu mbalimbali ili kujiongezea vyanzo vya mapato yao.

5. Pesa hailali
Unapaswa kutambua kuwa pesa haina saa, mapumziko wala likizo. Pesa hukaa na watu wenye bidii ya kazi. Jiongezee muda wa kufanya kazi zaidi, hasa katika biahsara yako binafsi au kazi utakayolipwa zaidi kwa kadri ya muda unaotumia kuwepo kazini.


6. Itendee pesa kama mpenzi mwenye wivu
Kama unataka kupata utajiri na uitwe mtu tajiri unatakiwa kuipa pesa kipaumbele. Pesa ni mfano wa mpenzi mwenye wivu. Ukiipenda itakupenda, usipoipenda itakudharau na kwenda kwa anayeithamini.

7. Umasikini hauna maana
Ondoa mawazo na fikra potofu kuwa, si jambo baya kuwa maskini, Hakuna mwanadamu anayependa kuwa maskini, kama wewe ni binadamu timamu unatakiwa kupenda utajiri na kuuchukia umaskini. Usipoteze muda wako kufikiria au kusoma jambo lolote linalohusu umaskini, “furaha haipatikani kwa kuutafakari huzuni”. Hebu tafakari usemi wa Bill Gates aliosema, “If you’re born poor, it’s not your mistake. But if you die poor, it is your mistake.” Akimaanisha kuwa “Kama umezaliwa maskini , sio kosa lako. Lakini kama utakufa maskini, hilo ni kosa lako”.

8. Pata mshauri (mentor)
Ni jambo la busara kumtafuta mshauri ambaye ni millionea, ili upate muongozo bora, katika safari yako ya umillionea. Kama huwezi kumpata mshauri aliyepo karibu yako, mchague millionea yeyote duniani na uanze kumfuatilia kwa kusoma na kufuata ushauri wake.


9. Iache pesa ikufanyie kazi
Uwekezaji ndiyo mbegu bora ya utajiri. Utaweza kutengeneza pesa nyingi sana kupitia uwekezaji kuliko mfumo mwingine wowote. Na kama hauna pesa ya kutosha utashindwa kuwekeza, kwakuwa uwekezaji unahitaji pesa ya kutosha hasa kama unataka mapato makubwa.

10. Lenga kupata million 10 na sio Millioni 1
Moja ya makosa makubwa yanayofanywa na wengi kifedha, ni tabia ya watu kuwa na malengo madogo. Nakushauri upende kuwa na mawazo makubwa hasa katika suala la kifedha.
Fuata hatua hizo 10 zitakusogeza kwenye utajiri. Epuka njia za kupata utajiri wa haraka, kuwa mwaminifu, usikate tama na ukifanikiwa, wasaidie wengine.