MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

TANZIA: MWANAMKE WA KWANZA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA, ANNA SENKORO AFARIKI DUNIA


DAR ES SALAAM: Mwanamke wa kwanza kwenye Historia ya Tanzania kugombea urais, Dkt. Anna Claudia Senkoro ameaga dunia Januari 4, 2016 asubuhi.
Senkoro aliyegombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha APPT-Maendeleo,  akichuana na rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2005, inadaiwa aliugua ghafla usiku wa kuamkia leo na amefariki baada ya kukimbizwa hospitali asubuhi ya leo.
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbuili imethibitisha kuupokea mwili wa marehemu Senkoro na imeelezwa kuwa msiba huo upo nyumbani kwake, Tabata Segerea jijini Dar.
Matokeo ya Urais 2005
Jakaya Kikwete (CCM)
9,123,952
80.28%
Ibrahim Lipumba (CUF)
1,327,125
11.68%
Freeman Mbowe (CHADEMA)
668,756
5.88%
Augustine Mrema (TLP)
84,901
0.75%
Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi)
55,819
0.49%
Christopher Mtikila (DP)
31,083
0.27%
Emmanuel Makaidi (NLD)
21,574
0.19%
Anna Senkoro (APPT-Maendeleo)
18,783
0.17%
Leonard Shayo (MAKINI)
17,070
0.15%
Paul Kyara (SAU)
16,414
0.14%