MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

WIMBO WA GOSPO WAPIGWA MARUFUKU NCHINI KENYA,NI UNAOSEMA YESU NIPE NYONYOMwimbaji Wa Muziki Wa Injili Nchini Kenya Anayefamika Kwa Jina La SBJ Amepigwa Marufuku Kuimba Wimbo Wake Wa Yesu Nipe Nyonyo.

Kwa Mujibu Wa Bodi Ya Filamu Nchini Kenya Imesema Wimbo Wa Yesu Nipe Nyonyo Haukutumia Lugha Fasaha.

Pia Mkuu Wa Bodi Ya Filamu Nchini Kenya Ezekiel Mutua Amesema Baadhi Ya Waimbaji Wa Kenya Wamekosa Maadili Na Kutumia Vipaji Vyao Kutunga Nyimbo Zisizo Kuwa Na Maadili.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kuanisha Filamu (KFCB) Ezekiel Mutua amekashifu vikali wimbo “Nipe Nyonyo” ambao umekuwa maarufu nchini katika muda wa majuma kadhaa sasa.

Umaarufu wa wimbo huo umetokana na sababu za kibishi hasa kutokana na kuwa ulifaa kuwa wimbo wa injili.Lakini wimbo huo una msitari ambayo inashtua ambapo mwimbaji huyo anayeitwa SBJ anamwomba Mungu ampe ‘nyonyo’, kumaanisha matiti.

Sehemu ya wimbo huo inasema "Eh baba nipe nyonyo, eh Yesu niko tayari,"
Haijulikani kwanii wimbo huo haukupigwa maruuku hapo awali Ingawa ulitolewa miaka kadhaa iliyopita,sasa hivi ndio hivi ndio umekuwa maarufu katika mtandao wa Youtube.
Mutua amekashifu wimbo huo na kuongeza kuwa baadhi ya wanamuziki wanatumia nyimbo za injili kuendeleza jumbe za kukufuru.
Alisema wimbo huo unaendelea kukaguliwa kwa sababu Wakenya wamekasirishwa:"Nashangaa sana mtu mzima anakaa chini na kuimba wimbo kama huu,Wasanii wetu wamejua kuwa kama hawaongei uchafu ama kutoa video za utata hawatasikilizwa wala kutazamwa na wanafanya hivyo ili wapate umaarufu”
Aidha Mutua Amesema Katiba Ya Kenya Hairuhusu Wasanii Kutunga Nyimbo Za Kudhalilisha Imani Au Utu Wa Mtu.

Tayari bodi hiyo ilikua kwenye mipango ya kuwaandikia Youtube ambao ndio wanamiliki wa mtandao huo ili waiondoe hiyo video kwasababu bodi hiyo inayo mamlaka na katiba haitakubali Wasanii kutunga nyimbo za kudhalilisha imani.


Mpaka sasa wimbo huo bado upo kwenye mtandao na umeshatazamwa mara 127,103 mpaka sasa.

AOMBA MSAMAHA KWA JAMII