RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

05.02.2017: BISHOP SAM OWUSU KUTOKA GHANA AWABARIKI WAUMINI WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI KATIKA IBADA YA SUNDAY TO REMEMBER

Hakika Mungu aliweza kuonekana katika ibada ya Sunday To Remember ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni. Jumapili ya 05.02.2017 Mungu aliweza kumtumia mtumishi wake Bishop Sam Owusu kutoka Kaneshie Accra Ghana kuhubiri habari njema katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Ibada hii ilianza saa 12 asubuhi na kumalizika saa 12 jioni. Katika ibada hii kulikuwa na Neno la Mungu, Maombezi, Kupakwa mafuta, watu wa kwanza walipokea zawadi kutoka kwa Malaika kwa imani kama Bishop Gertrude Rwakatare alivyowajhakikishia waumini wakanisa hili kuwahi na watapokea zawadi kutoka kwa Malaika wenyewe, uimbaji, kupita katika birika la BETSAIDA, maombi ya watu binafsi.

Mungu aliweza kuonekana kwa njia ya ajabu sana kwa watu waliofika katika ibada hii. Mungu alikuwa akiwahudumia watu wake kwa njia azijuazo Yeye. Tuliona watu wakiwa na sura za furaha wakiashitria kuwa walikuwa wakipokea kile ambacho Mungu alikuwa akikiachilia kupitia watumishi wake.

Nachotaka kukuambia ni kwamba endelea kufuatilia post zetu wakati na sisi tunaendelea kukuandalia mahubiri ya Bishop Sam Owusu kutoka Ghana. Ubarikiwe na Bwana..