RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

05.02.2017: MCH. FRANCIS MACHICHI ZSEMA BAADA YA AIBU ULIYO NAYO KUNA HATIMA JEMA MBELE YAKO SIKU YA JUMAPILI YA BIG SUNDAY TO REMEMBER


Katika ibada ya BIG SUNDAY TO REMEMBER siku ya Jumapili 05.02.2017 Mch. Francis Machichi alikuwa na haya ya kusema, “Nataka kuongea hivi baada ya aibu uliyo nayo hatima yako ni njema mbele za Mungu. Tusome Waamuzi 11: 29-30 inasema, Ndipo roho wa Bwana akamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase akapita na katika Mispa ya Gileadi na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni. Naye Yeftha akamuwekea BWANA nadhiri. Kwa nini Yeftha aliweka nadhiri? Nachotaka kukuambia, baada ya aibu uliyo nayo kuna hatma njema iliyopo mbele yako. Tuanze na nadhiri kwa sababu Yeftha alikuwa na sababu iliyoweza kuweka nadhiri. Mtumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anaposema, ”Wewe unatampa Mungu nini mwaka mzima.” Angalau mwambie BWANA mwaka huu 2017 nataka nadhiri yangu kwako ukinilinda na familia yangu, ukinitunza, ukinibariki, nitakutolea. Hii inaitwa NADHIRI, ambayo unakitamka kwa ajili ya BWANA unataka unamwangalia BWANA atafanya juu yako. Sasa nataka nikwambiem kwa nini Yeftha alifika mahali hapa akafanya nadhiri. Ukisoma Waamuzi 11:1 Basi huyo Yeftha Mgileadi alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba kwa wana wa Israeli, huyu Yeftha ambaye alikuwa ni shujaa sana. Ukiwa mtoto wa kahaba wewe hufai lakini Biblia inasema alikuwa ni shujaa lakini ndani ya ushujaa uliokuwa ndani yake alikuwa na aibu. Maana ya jina Yeftha ni “Mungu atafungua pamoja.” Alizaliwa kwa kahaba lakini ndani yake kulikuwa na mpango wa Mungu wa kufungua kitu mbele yake katika maisha yake ya kesho ndio maana nasema baada ya aibu uliyo nayo kuna hatima jema mbele yako.

BWANA ANAWEZA KUKUTOA KATIKA AIBU YAKO NA UKAONEKANA WA THAMANI
Biblia inasema, Yeftha ambaye alikuwa ni shujaa alizaliwa na kahaba na baada ya kuzaliwa na kahaba ndugu zake wakaanza kumpiga vita wakisema, “Hautarithi kitu kwa sababu wewe umezaliwa na mwanamke mwingine”, ilikuwa ni uchungu kwa Yeftha. Mungu atafungua, watu wakukusadia, hata kama wanakuona kwenye hali ngumu, watu hawatakuelewa lakini Mungu atafunguanjia. Yeftha akakaa katika nchi ya Tobu, na watu Wabaeadhuli walikwenda na kutangamana na Yeftha, wakatoka kwenda pamoja naye. Ikawa baadaye wana wa Amoni wakapigana na Israeli. Ikatukia hapo wana wa Amoni walipopigana na Israel, wazee wa Gileadi wakaenda kumtwaa huyo Yeftha katika ile nchi ya Tobu. Wakamwambia Yeftha, njoo wewe uwe kichwa chetu ili tupate kupigana na wana wa Amoni. Yeftha akamwambia wazee wa Gileadi Je, Ninyi hamkunichukia mimi na kunifukuza nitoke katika nyumba ya baba yangu? Basi kwanini kunijilia hivi sasa wakati mlio katika taabu? Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, kwa ajili ya hayo sasa tumegeuka, waliokuona unaaibika watakuona umegeuka kwa sababu masaa ya Bwana yamewadia. Wazee wakamwambie kijana ni kweli ulifukuzwa lakini sasa majira yamewadia tumegeuka, tulivyoongea vibaya kinyume na wewe, hata wale wanaokwambia haujapata mtoto umechelewa wewe waangalie tu maana muda umewadia watageuza wataanza kuongea vizuri kwa jina la Yesu. Sasa tumegeuka kukuelekea wewe tena ili uende pamoja nasi na kupigana na wana wa Amoni, nawe utakuwa kichwa chetu juu ya wenyeji wote wa Gileadi. Bwana anaenda kukuinua utakuwa kichwa katika familia yako.

UTAKACHOKIFANYA MWAKA HU2017 BWANA ATAKUWA NAWE ATAKUONDOLEA AIBU ULIONAYO
Biblia inasema katika kitabu cha waamuzi, basi Yeftha akawambia wazee wa Gileadi kwamba, mwanirejeza kwetu tena ili kupigana na wana wa Amoni, naye Bwana akiwatoa mbele yangu, Je, Mimi nitakuwa kichwa chenu? Tena watu wasikubembeleze wakisema wewe utakuwa mkurugenzi wetu, unaitawala familia pamoja na aibu uliyokuwa nayo, hatima yako ni kubwa sana mbele za BWANA. Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha “Yeye Bwana atakuwa shahidi kati yetu, tutafanya sawasawa na Neno lako. Hautalala tena, hautalia tena, utakacho kisema kitafanyika. Nami nakuambia utakacho kifanya kuanzia leo lazima BWANA atakutendea, utakacho tamka mwaka huu 2017 BWANA atakitenda maishani mwako. Naona watu wakifunguliwa, naona BWANA akibariki maisha yako. Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi na hao watu wakamfanya awe kichwa, tena mkuu juu yao, naye Yeftha akanena kwa maneno yake yote mbele ya BWANA huko Mispa. Naona watu wakikufanya wewe uwe kichwa katika familia yako, jamii yako, ofisini kwako,kazini kwako kwa jina la yesu…. Pokea

KERO INAMNYIMA MTU RAHA, NA DAWA YA KERO SIO KUWA NA PESA
Kero inamnyima mtu raha, na dawa ya kero sio kuwa na pesa, unaweza kuwa na pesa lakini unakero na dawa ya kero sio kujulikana na watu wakubwa lakini dawa ya kero ni maombi. Mtumishi Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alisema ukifika asubuhi mapema kutakuwa na malaika ambao watakuwa wanakushughulikia imani yetu. Mara nyingi alichokitamka mtumishi wa Mungu huwa kinatokea kwenye maisha yetu. Unajua mambo ya rohoni hayatendeki kwa macho ya mwili, bali yanatendeka katika ulimwengu wa roho. Inapotokea kero kunakuwa na adui upande wa pili, Biblia inasema Hanna alikuwa ananyanyasika sio na mume wake bali na Penina, Nuhu kwenye safina hakusumbuka kwa ajili ya mke wake na watoto wake Hamna. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ametufundisha akisema kulikuwa na kero huko ndani maana milio ya wanyama, harufu, kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ilikuwa ni kero. Kwa hivyo hivyo vitu vinaletwa na adui, kuna mtu anakunyima raha ndani ya moyo wako anakukera anaitwa shetani na shetani hatumuoni kwa macho ya mwili bali tunamgundua hila zake kupitia ulimwengu wa roho. Shetani mara nyingi hutumia watu au vitu kukuletea kero ili ughadhabike {uchukie} na mwisho wake utende dhambi kwa sababu unaweza kuchukua maamuzi mabaya kutokana na hasira ulizonazo baada ya kukerwa na yule aliekukera. Ninacho kusihi ni kumuomba Mungu usipatwe na hasira yeyote ile ikakusababishia kuingia jehanamu. 
unaweza ukawa na pesa lakini ukuwa bado umezungukwa na kero mbalimbali ambazo zinaweza kukusababishia madhara mbalimbali na pesa yako isikusaidie. Ubarikiwe



 Mch. Francis Machichi

Mch. Stanley Nnko (kushoto) na Mch. Noah Lukumay (kulia)