MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

12.02.2017: HAPA KWAYA NA JOYBRINGER KWAYA ZA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" ZILIVYOWABARIKI WAUMINI SIKU YA JUMAPILI

Mungu azidi kuwatunza, kuwalinada , na kuwaheshimisha waimbaji hawa wa kwa ya Joybringers na Happy Kwaya. Kila kuitwapo leo wanazidi kutubariki kwa uimbaji wao. Mungu ameweka kitu ndani yao na kuwapaka mafuta ya kitumishi. Siku ya Jumapili 12.02.2017 watu wengi sa walionekana kubarikiwa na uimbaji wao kwa jinsi walivyokuwa wakijituma kwa kazi ya Mungu. Nyimbo zao zimekuwa na nguvu ya ajabu sana pale usikiapo. Pia Mungu amewapa hekima ya upole na unyenyekevu wakiwa katika huduma na mahali utakapokutana nao. Kama Wakristo tunapaswa kuwaombea kwa huduma yao na pia maisha yao yakawe bora kila kuitwapo leo.

Tukualike na wewe katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 jioni kutakuwa na ibada maalum kwaajili yako na maisha yako kwa ujumla. Bwana atabadilisha historia ya maisha yako. Mungu akubariki na akusaidie Jumapili hii usikose Nyumbani Mwa Bwana.