MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

12.02.2017: MCH. NOAH LUKUMAY ACHUKIZWA NA UMASKINI ASEMA UNAMSABABISHIA MTU KUPATWA NA AIBU KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

UKIFANYA BIDII KATIKA KUMSIFU BWANA ITAKUFANYA UMUONE MUNGU WETU WA MBINGUNI
Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 12.02.2017 katika ibada ya KUONDOLEWA AIBU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” alikuwa na haya ya kusema, “Neema ya Bwana ipo mahali hapo ulipo. Neno linasema, ”Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona”, bidii yako katika kumsifu Mungu ndio inakufanya umuone yeye, bidii yako ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli ndio itakufanya umuone yeye, bidii yako ya kuacha ya dunia na kumwangalia yeye ndio itafanya ashuke katika maisha yako.Sasa naomba uinue mikono yako na sema, “Ee BwanaYesu, niko tayari, kutana na maisha yangu, maana bila wewe mimi siwezi, Ee Bwana Yesu ibada hii ya sifa ninakupa wewe peke yako, sina mwingine katika maisha yangu, Ee Bwana Yesu, moyo wangu wote, mawazo yangu yote, ninapoenda kukusifu nione majibu ya maisha yangu katika jina la Yesu”. Baada ya hapo Mch. Noah Lukumay aliweza kuomba, alisema, “Asante Bwana Yesu kwa sababu umesikia kilio changu, umeyaona mateso yangu na asubuhi ya leo ni asubuhi ya utukufu wako, Ee Bwana Yesu simama nasi leo kwa utukufu wako katika jina la Yesu..Ameni”

HATA KAMA KUNA AIBU YA AINA GANI ACHA KUSIKILIZA SAUTI ZA WATU
Hata kama kuna aibu ya kiasi gani imekuja kwenye maisha yako acha kusikiliza makundi ya watu ambao wako kinyume chako maana hawana cha kukusaidia, angalia yupi ambaye yuko upande wako anataka akusogeze mahali ambapo unataka kufika. Inua mkono wako na sema, ”Kundi lolote ambalo liko kinyume changu, leo nakuachilia kwa jina la Yesu Kristo, kundi la aibu leo nalikataa kwa jina la Yesu.” Kila mtu ana mahali anapitia, kila mtu anamsiba wake, anakilio chake. Kuna mahali unapita unajiuliza, “Hivi Mungu kaniacha ama yuko na mimi?” Nataka nikwambie “Hata kama unaonekana kama umepotea, Mungu anaangalia mahali umeshindwa ili aonekane katika maisha yako, Mungu haaangaliagi mahali umeshinda, anaangalia mahali umeshindwa. Yeye ni Mungu wa mbinguni. Sasa wanaosherekea aibu yako, watasherekea ushindi wako, Bwana Mungu hata kuacha wala hata kupungukia. Leo huna watoto lakini kesho yako inakuja utakuwa mama wa watoto wengi kama unaamini sema, ”Napokea.” Aibu yangu ndio miguu ya Mungu kukufuata, aibu yako ndio hatua ya Mungu kukusikiliza, wakati pale watu wanakung’onga, ukitembea unadhani ukosawa kumbe wanaminyana na kukusema, nami nasema, “Wataminyana sana majira yanakuja Jehova atawapiga upofu macho yao na wataabika wao. Maandiko yanasema, ”Bwana anaangalia vilivyodhaifu ili aviinue ili viheshimike.” Waliokuona unapigwa mawe Yesu ameshaona. Katika Biblia yule mwanamke aliyekuwa amefumaniwa walidhani watammaliza wakanyanyua mawe, wakasahau Yesu ni mawe mwenyewe, wakasahau mawe sio ya kumuumiza, mawe yale ni ya kumtetea, fimbo wanayokuadhibu nayo itakuwa furaha, itakuwa ushindi katika maisha yako.

NI WAKATI WA BWANA KUTUTETEA DHIDI YA MAADUI ZETU NA KUTUONDOLEA AIBU
Watu wengi sana wameabishwa na mambo mengi sana, na wengine ni kutokana na umaskini wao, nami leo natangaza kwa jina la Yesu, umeaibishwa vya kutosha, naona vazi la heshima, naona vazi la utukufu katika jina la Yesu. Katika Biblia, yule mwanamke alivyokuwa ameokolewa mawe kwa sababu amefumaniwa walisahau kwamba lile jiwe ni Yesu mwenyewe, walipochukua lile jiwe wakati wanatembea walipolipiga kwa jiwe jiwe likaongea, jiwe likasema, ”Huyu mwanamke mbona hatuwezi tukampiga, sisi tumeletwa kumtetea huyu mwanamke kama nyie mmejiandaa na nguvu zenu hili jiwe haliwezi kung’oka.” Badala ya jiwe kumdongokea yule mwanamke, likadondokea kwenye miguu ya maadui zake. Chochote wakusemacho kwa jina la Yesu watamalizwa na hichohicho. Ni wakati wa Bwana kukutetea mwambie jirani yako “Bwana atanitetea, mimi sio wa kuaibia Mungu wangu atanitetea wanao sherekea kuaibika watasherekea ushindi wangu Bwana atawaaibisha, wanaodhani hutavuka wataona uko ng’ambo kwa jina la Yesu.” Usiwasikilize wapinzani hawana jema kwako, wao wanatengeneza makosa, umevaa vizuri watasema, “Sio rangi yake”, umevaa nguo hii wanasema, “Imekuwa ndefu sana.” Hawawezi kuona jema kwako na hawajui kuwa wanapoona jema kwako, Mungu anainuliwa. Unajua kila kitu kizuri kina vita vyake, ukiona wanakufuatilia ujue kuna cheo kikubwa mbele yako, jua kuna hatua utashinda ndio maana wanataka kukuaibisha kwa sababu wewe ni pekee ndio maana wanataka kushindana na wewe kwa sababu nguvu zako sio za kwao, hatua zako sio za kwao, namuona Jehova akikuinua zaidi. Amen

WAACHE WAKAE VIKAO VYAO KUKUABISHA , LAKINI MUNGU ATAKAA NA WEWE
Kuna watu wanatamani kukuona wewe unaishi maisha ya kinyonge, wanatamani kuona unaabika katika jamii yako, nasema, wacha wakae vikao vyao wakusemea mabaya na kukusengenya, lakini Bwana atakaa kikao kwenye chako akitakia mema na mafanikio. Walikaa kikao juu yako wakisema, “Tunammaliza, hafai”, kumbe kikao hicho cha duniani kimekuwa double kule juu mbinguni. Wewe usiogope mtu akikufanyia kikao hapa duniani cha kukufedhesha, wewe unatakiwa upige goti mbele za Mungu na usema, “Najua Bwana anatengeneza njia kwa ajili yangu.” Wakati wanakusengenya achana nao wewe songa mbele, wakati wanakurushia mawe wewe songa mbele. Unatakiwa “Kujitambua.” Mzazi wako aliyekuzaa hawezi kuruhusu uaibike, Mungu yeye ametukomboa hawezi ruhusu tuaibike, mwenye haki ataanguka mara saba lakini atainuka. Biblia inasema, “Usifurahie ewe adui yangu maana nikianguka Bwana atakuwa kimbilio, Bwana atakuwa msaada, Bwana atakuwa shujaa wangu, Bwana atakuwa furaha yangu.” Wanaochekelea matatizo yako waongeze kicheko baada ya kuchekwa kunakuinuliwa kuna heshima kwa jina la Yesu, utaisahau aibu ya ujana wako. Kumbuka hapo unapopita ni hatua, utafika uendako kwa kishindo. Leo nina matope lakini sitoishia na matope, leo nimekaa chini lakini sitoishia chini. Usione nimenyamaza naandaa nguvu za kupanda juu, ukiniona utadhani sina mwelekeo kwa sababu kwa Jehova kuna kitu anatengeneza. Ukiona kimya kikubwa ujue kuna kishindo kikubwa, Sema kwa jina la Yesu leo aibu inaongoka kwa jina la Yesu.

SEKUNDE MUNGU ANAWEZA KUKUONDOLEA AIBU YAKO NA KUITWA MTU THAMANI
Yawezekana unaishi maisha fulani ambayo hutamani kuyaishi, umekuwa ni mtu ambaye unasimagwa na watu kutokana na hali uliyonayo. Naomba useme maneno haya, sema, “Kwa jina la Yesu hakuna sindano itakayo inulikwa kinyume changu, nitafanikiwa kwa jina la Yesu na wanaonisema vibaya yawarudie wao.” Yeyote aliyekutelekeza ili uaibike mpe pole nyingi maana anakwenda kuaibika mbele yako. Nataka nikwambie hivi “Chochote kilicho inuka ili kikumalize sema pole maana hicho kilichokuumiza, kilichokuliza machozi, kimekufanya ukaona kama hutofanikiwa kitaenda kuwa muujiza wako, kinaenda kukupa mama wa familia kubwa.” Mahali ambapo shimo limechimbwa hilohilo shimo litakupeleka mahali pa juu zaidi, hilohilo shimo litakufanya heshima kwa jina la Yesu. Katika Biblia watu hawakujua yule mtumwa alivyouzwa kuwa baadae atakuwa waziri. “Kuna mahali wamekuuza lakini wamekuuza kuwa chombo kikubwa, walidhani wewe ni mtumwa lakini unapoenda hatua moja hatua zako zinabadilika unatoka kwenye utumwa unakuwa Manager.” Ninaona watu wakibadilishiwa mavazi yao, nguo zao, nyumba zao, marafiki wema na marafiki wanaokutesa, wanaokuumiza wanaondoka kwenye maisha yako, wataachia biashara yako, halafu utaenda mahali sahihi . “Unatoka kwenye aibu unaingia kwenye utukufu, unatoka kwenye kuzalilika unaenda kwenye kuheshimika.” Wapendwa hali unapitia si mahali pa mwisho ni mahali pa kwenda juu zaidi, umeshuka chini lakini haina maana umemalizika, unaenda kulipuka zaidi ya siku zote sema, “Napokea kwa jina la Yesu.” Roho ya aibu haina nafasi kwangu. Mungu akusaidie kwa Jina la Yesu Kristo..

TUNAKATAA KILA ROHO YA AIBU KATIKA MAISHA YETU KWA JINA LA YESU
Aibu yoyote itakayokuja kwenye safari yangu na yeyote anayevamia safari yangu ya mafanikio, ataabishwa yeye mwenyewe kwa jina la Yesu na ajue atakuwa ananivisha taji la Ushindi bila yeye kujua kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa maadui wote wanaojianda niabike wanaonisemea maneno mabaya, Bwana anakwenda kuwavuruga katika vikao vyao. Sema, ”Kwa jina la Yesu, roho ya aibu popote ulipo achia watoto wangu na maisha yangu kwa jina la Yesu.” Sasa anza kukemea roho ya mapepo, aibu ya magonjwa mabaya, madeni, matatizo kila vifungo vya kila namna, aibu kwenye familia, aibu ya mume, aibu ya mke katika jina la Yesu aibu ya mafarakana. Leo tunakata kwa jina la Yesu Kristo, nakataa kila roho ya aibu inayofuatilia maisaha yangu kwa jina la Yesu, kila aibu iliyotumwa kwa watoto wetu, aibu ya taraka, aibu ya kazi, aibu ya kutokuzaa tunaikataa kila aibu kwa jina la Yesu, kila aibu inayoelekezwa kwenye maisha yatu tunaikataa kwa jina la Yesu. Sema, “Kwa jina la Yesu roho yoyote inayotoka kwenye aibu ambayo inanifuatilia kwenye ufahamu wangu kwenye kichwa changu, achia leo kwa jina jina la Yesu.” Wengine ndoto zina watesa, unaota unagombana na mume wako na inatokea, unaota unapata mimba na inatoka hiyo ni roho ya aibu, unaota kuna vitu vinakufuatilia. Sema “Kwa jina la Yesu ewe shetani toka”. Sema, “Ee Bwana Yesu chochote ambacho kimeingia katika tumbo langu ili kuleta roho mbaya leo iondoke katika jina la Yesu.”