RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

12.02.2017: WATU WAZIDI KUMIMINIKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" NA KUOKOKA...HAWA WALIOKOKA JUMAIPILI

Hawa ni baadhi ya watu waliofika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 12.02.2017 na kuamua kuokoka kwa hiari yao wenyewe. Huu ni uamuzi sahihi waliochukua wa kuanza maisha mapywa na Bwana kwa mwaka huu wa 2017. Mch. Francis Machichi aliweza kuwaita madhabahuni kwaajili ya kuombewa watumishi wa Mungu na pia kuwakabidhi mikononi mwa Bwana. Mch. Mama Mgetha na Mch. Francis Machichi waliweza kuwaongoza sala ya toba na baadae kuwaombea. Ibada ilipomalizika tu waliweza kubatizwa na maji mengi na siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".


Ndugu yangu wewe ambaye hujaokoka bado, sauti ya Mungu inakuita "NJOOO" kwa Yesu leo. Huu ni muda wako wa kuokoka, umemtumikia shetani sasa yatosha, mateso unayopitia ni shetani tu anakutesa. Mungu anakupenda sana, natamani kukuona ukichukua hatua na kuja kwa Bwana siku ya leo.

Kama Roho wa Bwana ameshaongea na wewe sana, nakualika katika ibada ya Jumapili hii Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Watumishi wa Mungu watakuombewa na utabatizwa kwa maji mengi. Mungu akubariki sana


Mch. Mama Mgetha akiwaongoza sala ya TOBA waongofu wapya




 Mch. Francis Machichi akiwaombea watu walioamua kuokoka siku ya Jumapili