MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

19.02.2017: BEATRICE MWAIPAJA ATOA UJUMBE MZITO KUPITIA UIMBAJI WAKE KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA KUTOKA KATIKA UTUMWA ILIYOFANYIKA MLIMA W MOTO MIKOCHENI "B"

Katika waimbaji waliobahatika kuimba katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"  na wakakonga mioyo ya watu na kuacha watu wakiwa na hamu ya kurudiwa wimbo uliokuwa ukiimbwa mmojawapo ni Beatrice Mwaipaja. Jumapili 19.02.2017 mtumishi wa Mungu Beatrice Mwaipaja aliweza kupanda katika madhabahu ya Mungu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na kuanza kuimba wimbo wake ulionekana kuwa na upako wa ajabu sana. Ile anaanza kuimba tuliona uwepo wa Mungu ukitanda katika kanisa hili, watu walikuwa kimia wakisikiliza ujumbe uliokuwa ukiingi mioyoni mwao na kuponya Roho zao, na baadhi yao walishindwa kujizuia wakaamua kusimama na kucheza huku masikio yao na akili zao zikifuatilia kile anachooimba. Hakika wimbo wake ulifanya watu kuendelea katika na ile hali ya hofu ya Mungu. Mungu azidi kumbariki mtumishi wake Beatrice Mwaipaja.
Beatrice Mwaipaja

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Beatrice Mwaipaja

Beatrice Mwaipaja

 Beatrice Mwaipaja