MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

19.02.2017: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA ZAFANYIKA BARAKA SIKU YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI “B”

Siku ya Jumapili 19.02.2017 tuliweza kupokea upako wa tofauti sana kupitia uimbaji kutoka kwa Happy Kwaya na Joybringers za Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Nachotaka kusema ni kwamba, kuna kitu ambacho Mungu amekiweka kwa waimbaji hawa , wamefanyika Baraka katika kanisa hili na pia kwa watu waliobahatika kusikia nyimbo zao. Ni waimbaji ambao wamejitoa kufanya kazi ya Bwana wakiwa bado vijana. Na Mungu amekuwa mwamini kwani kupitia uimbaji wao tunaona nguvu za Mungu zikitugusa kwa njia moja au nyingine. Jumapili hili walisababisha watu kukaa kimia kanisani wakati wakiimba, kwani ujumbe wao ulikuwa unapita katika masikio ya watu na kiingia katika mioyo ya watu. Kuna watu walipona mioyo yao kupitia uimbaji wao na kucheza kwao. Nasi tuna kila sababu ya kuwaombea hawa waimbaji ili Mungu asiwaache wakarudi nyuma, kwa maana kurudi kwao nyuma kunaweza kusababisha kundi kubwa kurudi nyuma na hasa wale waliowafuatilia katika huduma yao ya uimbaji. Tunahitaji kuwatia moyo kwa maombi ili Mungu azidi kuwalinda katika maisha yao, afya zao, familia zao n.k.


Wewe ambaye hukubahatika kufika katika ibada hii ya KUONDOKA KWENYE UTUMWA tunakualika katika ibada ya Jumapili hii itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa, utaona magari ya Mlima wa Moto Mikocheni “B” au utasikia watu wakisema “Kanisani kwa mama Rwakatare”. Mungu na akubariki sana.