RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

19.02.2017: WANANDOA WAMSHUKURU MUNGU KUPATA MTOTO KATIKA IBADA YA JUMAPILI MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Bwana harusi alikuwa na haya ya kumshukuru Mungu siku ya Jumapili 19.02.2017, alisema, Bwana Yesu asifiwe. Tunamshukuru Mungu wa mambo makubwa aliyo tenda katika ya maisha yetu kupitia Dr. Gertrude Rwakatare. Tuliingia Mlima wa Moto Mikocheni “B” tukiwa vijana kabisa tukiwa single, lakini leo Mungu ametuongeza familia yetu kwa kutupa mtoto. Tuna kila sababu ya kutoa shukrani zetu kwa Bishop wetu ametupokea, akatufundisha, ametupa hekima tumeweza kutembea katika hiyo heshima. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya wachungaji wote, wazee wa kanisa, kanisa kwa ujumla na vijana wote kwa pamoja walisimama kiuaminifu kuweza kuomba kwa ajili ya familia yetu hakika tumemuona Mungu kutipia watu hawa katika maisha yetu. Baada ya hapo mke wa Bwana harusi alikuwa na haya ya kusema, “Bwana Yesu Asifiwe. Bishop nakupenda, tushukuru kwa kutupokea, kutuombea, nashukuru Mungu katika ujauzito wangu nilihudhulia kanisani nilikosa siku moja tu, ambayo Jumanne yake nikajifungua. Mungu alinisaidi kufika kwenye mikesha, nafanya usafi kanisani. Wakati wakujifungua sikujisikia uchungu, nilijifungua salama, lab nzima nilikuwa mimi na madaktari sita walionizunguka. Wakati wa kujifungua madaktari walishangaa na kusema “Haijawahi kutokea.” Kwahiyo nikambariki Bwana kwa sababu amenitetea. Namshukuru Mch. Elizabeth Lucas pamoja na kanisa la nyumbani pamoja na Mch. Noah Lukumay waliniombea kila siku wakikutana na mimi wananiombea wananitia moyo Mungu awabariki, na namshukuru Mungu kwa sababu ya mume wangu kipingi chote cha ujauzito alikuwa ananitia moyo nikiwa siwezi kupika ananisaidia namshukuru sana. Tunasadaka ya shukrani.